SIMBA CEMENT

SIMBA CEMENT
KAHAMA BRACH

ROCKEN HILL

ROCKEN HILL
KAHAMA

Wednesday, 17 May 2017

MWANAMKE KAHAMA AFUNGWA JELA MIAKA KUMI AKAMATWA NA MABOMU PINGU, VISU VYA KIJESHI

Moja ya Bomu la kutupwa kwa mkono aliokamatwa nayo Aisha juma mkazi wa kata ya  nyahanga wilayani kahama  Pingu ambazo alikamatwa nazo  Aisha  juma 

Risasi alizokamatwa nazo Aisha juma mkazi wa kata ya nyahanga wilayani kahama pamoja na mabomu ya kutupa kwa mkono

KAHAMA 
Mahakama wilaya ya kahama mkoani shinyanga imehukumu kifungo cha miaka 10  Aisha Juma kwa kosa la kuutwa na hatia ya kukamatwa na siraha mabomu ya kutupa na mkono pamoja  visu na pingu  katika kata ya  nyahanga. 

Akiongea mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo  Vodia Kiharuzi mwendesha mashitaka Athumani kisango aliambia mahakama hiyo kuwa Aisha juma alikamatwa maeneo ya nyahanga majira ya joni akiwa na silaha hizo.

Aidha mwendesha mashitaka aliambia mahakama aisha alikamatwa tarehe 11 mwezi wa kumi nyumbani kwake akiwa na silaha hizo,kwa mujibu wa sheria cha 21 cha mwaka 2015 ni kosa kukutwa na risasi.

 Akitoa  hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga,Evodia Kyaruzi alisema kuwa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ameridhika kuwa, mshitakiwa  walikutwa na mabomu hayo ya kinyume cha sheria na kumtia hatiani kwenda jela mika kumi .

Hakimu huyo alisema kuwa,mahakama hiyo baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote imeridhika nao, hivyo washitakiwa wanatiwa hatiani kwa kifungo cha adhabu ya sheria cha 21 cha mwaka 2015.

  Awali katika ushahidi wake Mwendesha mashitaka wa polisi upande wa Jamhuri,  Athumani kisango na upande wa mashahidi uliotolewa  mahakamani hapo waliiambia mahakama hiyo kuwa,mshitakiwa  walikutwa na mabomu hayo  katika eneo la nyahanga  .

Kwa upande wake  mshitakiwa   katika utetezi wake,alikana kukutwa na mabomu  hayo kuomba mahakama kupunguzia adhabu hiyo.

Awali katika kesi hiyo Mwendesha mashitaka wa polisi upande wa Jamhuri  Athumani kisango ,aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe kufundisho kwa jamii na watu wenye kujihusisha na biashara  za kuuza siraha.

Mwisho 

Thursday, 4 May 2017

MEI MOSI ILIYONDOLALA SHINYANGA WANANCHI WASHINDWA KUJITOKEZA KWA WINGI

 Mandamano 

KTC kahama mji walivyotia fola kwenye mandamano wakiongozwa na Afisa utumishi  

Baadhi ya watumishi 

 Baadhi ya wafanyakazi wa mingodi rai wa kigeni wakisherekea siku ya wafanyakazi Duniani 

magari ya wafanyakazi wakipita na kwa mgeni rasm Zainab Telack 

 Michenzo ilikuwepo igawa watu walikuwa wachache 
MKUU  mkoa wa shinyanga Zainab Teleck akihutubia kwenye siku ya wafanyakazi Duniani Kwenye uwanja wa ccm kabarange Wednesday, 3 May 2017

WORLD PRESS FREEDOM OF EXPRESSION KAHAMA JOURNALIST FORUM

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa kahama Abel shija akikabidhi vitu mbalimbali katika kituo cha watoto yatima katika siku ya vyombo vya habari Duniani hapo, umoja wa waandishi wa habari kahama kahama journalist forum 

Vitu  mbali mbali vilivyotolewa kwenye kituo cha  watoto yatima cha mvuma siku ya vyombo vya  Habari  Duniani ambapo kahama Journalist forum walitoa zawadi ya vitu mbali mbali 

Uga,mafuta juice pipipi vilitolewa 

Mwenye tisht ya ragi nyekundu ni katibu wa kahama journalist forum Salvatory Kelvin kwenye picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha mvuma.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa kahama Abel shija akikabidhiwa Risala na katibu wa kahama journalisst forum Salvatory Kelvin

Baadhi ya watoto yatima katika kituo  cha mvuma wilayani kahama 


Watoto wa kituo cha mvuma

KAHAMA 

 Waandishi wa habari wilayani Kahama mkoani Shinyanga  wameungana na waandishi wa habari wengine nchini na kufanya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Mratibu wa waandishi hao mjini humo Kahama journalist Forum  Salvatory Kelvin alisema wameamua kufanya maadhimisho hayo kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki mbili katika kituo cha watoto yatima cha Mvuma

Miongoni mwa  zawadi hizo zilizotolewa na waandishi hao ni pamoja na sukari, mafuta ya kula, sabuni ya unga, sabuni za vipande, dawa ya meno, juisi,biskuti pamoja na pipi  ambavyo thamani yake ni shilingi laki mbili na nusu

Friday, 14 April 2017

ADAKWA AKIMBA SANDAKA KANISANI

nduku cha sandaka ambapo wizi aliimba  sandaka 

hili ndiyo kanisa ambalo wauumi wake wakati wa kusali jemba moja likachota sandaka 

Wakati mchungaji na waumini  wa kanisa la EAGT (JERUSALEMU) lililopo kata ya majengo wilayani Kahama mkoani  Shinyanga wakiwa katika maombi mazito huku wakiwa wamefumba macho kama ulivyo utamaduni wa makanisa yanayojiita kuwa ya kiroho muumini mmoja alitumia fursa hiyo kuchota fedha za sadaka.

Tukio hilo la aina yake lililovuta hisia ya watu wengi limetokea jumapili april 9 mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni wakati mchungaji Gwamiye akiongoza maombi kwa waumini wake huku wakiwa wamefumba macho ndipo muumini  mmoja alijifanya anatoa sadaka kasha kuchota shilingi 2,000 ndani nduku.

Mmoja wa waumini wa kanisa hilo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema licha ya muumini huyo kudokoa shilingi 2,000, siku hiyo hiyo misa ya asubuhi muumini huyo alidakwa na mashemasi wa kanisa hilo baada ya kuchukua fedha isiyofahamika wakati alipoungana na waumini wengine kwenda kutoa sadaka ambapo hata hivyo alisamehewa.

“Huyu jamaa anayejiita kuwa ni muumini wa kanisa hili siku hiyo hiyo ya jumapili majira ya asubuhi alisamehewa na mashemasi wa kanisa hili baada ya kuchukua kiasi cha fedha ambacho ambacho walisema ni kikubwa bila kufafanua huku wakidai pengine alikosa fedha ya kujikimu kimaisha,” alisema muumini huyo wa kanisa la EAGT Majengo bila kutaja jina.

Hata hivyo baadhi ya waumini walidai kushangazwa na kitendo hicho cha vibaka kuanza kuingia katika nyumba mbalimba mbali za ibada kwa lengo la kuiba sadaka bila kumwogopa mungu.

Naye mchungaji wa kanisa hilo Felix Gwamiye alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo kanisani kwake na kusema kuwa kwa sasa kuna wimbi la vibaka wanaoingia ndani ya makanisa wakati maombi yakiendelea huku wakati wakiwa katika maombi mazito wao ndipo wanapata mwanya wa kudokoa fedha za sadaka.

Katika tukio hilo Gwamiye alitoa wito kwa makanisa ya kipentekostal wilayani hapa kukaa chonjo na vibaka wanaoingia kanisani na kujifanya ni waumini kumbe wanavizia sadaka za waumini.

“Mtuhumiwa huyo alikamatwa na mashemasi wakati alipomuona akiiba hela za sadaka baada ya waumini kumaliza kutoa sadaka na kuanza maombi, mimi kama kiongozi wa kanisa hili nimemsamehe lakini asithubutu kuingia katika makanisa yoyote hapa Kahama  maana waumini wakiamua kufunga novena ya maombi laana itamsumbua,” alisema Gwamiye.

Hata hivyo katika mahojiano yake na gazeti hili muumini huyo aliyejitamburisha kwa jina la Dismas Simoni(35) mkazi wa Kata ya Ushirombo wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita alisema kuwa ni shetani ndiye aliye mtuma na kujikuta anadokoa kiasi hicho cha fedha na kumuahidi kiongozi huyo wa kanisa kuteua watu wa kuongozana nao kwa ndugu yake hali ambayo ilimfanya Gwamiye amsamehe.

“Mimi ni mkazi wa kata ya Ushirombo Bukombe huku Kahama nimekuja kumtembelea kaka yangu anayeishi kitongoji cha Nyamhela kata ya Mhongolo binafsi niseme nimepitiwa tu na shetani samahani sana kama mtanisamehe naweza kurudisha hela niliyochukua asubuhi nah ii 2,000/= siewezi kurudia kosa jamani,” alisema mtuhumiwa wa kuiba sadaka.

Mwisho.

  

Sunday, 9 April 2017

DIWANI MTENDAJI WA KATA WAKIONA CHA MOTO BAADA YA WAKAZI KUFANYA OFISI YA MTENDAJI ENEO LA MAZIKO

 Baadhi ya wakazi wa kata ya mhongholo wakiwa wamebeba saduku la mtoto mchanga kuja kuzika katika ofisi ya mtendaji 

JENEZA LA MTOTO LIKIWA NJE YA OFISI YA MTENDAJI KWA  AJILI YA MAZIKO 

Diwani wa kata ya mhongholo mh michael  Mizubo akiwaomba wananchi kuwacha kufanya kitendo hicho 

hili ndiyo kaburi lilochimbwa katika ofisi ya mtendaji kwa tuhuma ya kuuza maeneo ya maziko yenye na diwani wa  kata hiyo 


Hili ndiyo kaburi na jeneza  kabla maziko na polisi walifika eneo hilo na kuwatawanya wanachi katika eneo hilo la ofisi ya mtendaji  Polisi baada ya kufika katika eneo hilo  la ofisi ya mtendaji wa kata ya mhongholo

Gari la polisi katika eneo la msimba 


KATIKA hali isiyotarajiwa na katika kuashiria kukomaa na kukithiri kwa migogoro ya ardhi wilayani Kahama, mkoa wa Shinyanga, wananchi wa mtaa wa Mhongolo, kata ya Mhongolo, wilayani hapa walitishia kuigeuza ofisi ya afisa mtendaji wa kata hiyo kuwa eneo la maziko.

Wananchi hao wakiwa wamejawa na jazba walifika ofisi za mtendaji wa Kata hiyo majira ya saa 7:00 mchana huku wakiwa wamebeba jeneza lililodaiwa kuwa na mwili wa kitoto kichanga cha umri wa mwezi mmoja kilichotambuliwa kwa jina la Rosemary Kanamba na kulazimisha kuchimba kaburi mbele ya mlango wa ofisi ya mtendaji wa kata hiyo aliyetambuliwa kwa jina la Maziku Mbusili.

Wananchi hao walidai kuchukua uamuzi huo kutokana na kile walichodai kuuzwa kwa eneo la makaburi walilotumia kuzika wafu wao miaka ya nyuma huku wakimnyoshea kidole diwani wa kata hiyo Michael Mizubo wakimtuhumu kuhusika kuliuza eneo hilo kinyume cha taratibu na bila idhini ya wakazi wa mtaa wao.

Mmoja wa wananchi wa Kata hiyo Jackson Mselemu akizungumza na wandishi wa habari waliofika katika tukio hilo alisema kuwa walichukua hatua hiyo baada ya kuzuiliwa kuzika nyumbani kwa baba wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Justine Kanamba ambapo uongozi wa Kata hiyo ulidai sheria haziruhusu kwa kuwa kata hiyo imo ndani ya Halmashauri ya Mji wa Kahama.

“Tumeheshimu mamlaka tumetafuta eneo la kuzika tumekosa lakini Mhongolo hapa tumekuwa na eneo lililokuwa mashamba ya Bega kwa Bega tangu miaka ya sabini na diwani wa Kata yetu analifahamu kwani ameongoza miaka kumi na sasa anaendelea kuongoza lakini yeye ndiyo anayefanya vikao vya siri vya kuendelea kuuza maeneo hayo tunamuomba mkuu wa wilaya Fadhil Nkurlu aingilie kati suala hili,” alisema Mselemu huku akiangua kilio.


Saturday, 8 April 2017

USHETU WAKABIDHI MAJENGO YA MAKAO MAKUU KWA MJI HUKU YAKIWA YAMECHAKAA


LICHA ya halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga kukiri kukabidhiwa majengo yaliyokuwa yakitumiwa na hamlamashauri ya Ushetu kama ofisi wakati wakiendelea na ujenzi wa makao makuu huko Nyamilangano lakini majengo hayo yamekabidhiwa rasmi yakiwa yamechakaa huku madirisha ya vioo yakiwa yamevunjwa na watumishi wake hali ambayo nyaraka za ofisi zimezagaa na kuoneka holela.

Hali hiyo ilielezwa na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama, Abel Shija wakati akizungumza na wandishi wa habari muda mfupi baada ya kamati ya fedha na uchumi kufanya ziara ya kukagua miundo mbinu ya majengo waliyokabidhiwa na kujionea uharibifu uliofanywa na watumishi wa halmashauri hiyo baada ya kugundua wanaondoka huku wakitakiwa kuziacha nyaraka zao.

Shija amewambia wandishi wa habari kuwa kulingana na majengo hayo yaliyokabidhiwa na halmashauri ya Ushetu kwa mji ukarabati wake wake  unahitaji kiasi kikubwa cha fedha hali ambayo  halmashauri itaingia hasara kubwa katika ukarabati wa miundo mbinu wa majengo hayo.  

“Kwa usahihi wa jambo hili kwanza tuishukuru sana serikali kupitia Tamisemi ka sababu imeliona jambo hili lakini pia imewezesha tufante usafi na ukarabati mapema wa majengo haya yaliyokuwa yametelekezwa   pamoja na kurejesha majengo haya yaliyokuwa hapo awali yakitumika kama majengo ya halmashauri ya wilaya ya Kahama na baadaye baada ya kupatikana kwa halmashauri tatu za Ushetu, Msalala na Mji yenyewe, licha ya kukabidhiwa majengo haya wameyaharibu sana kwa kuyachakaza,” amesema Shija mwenyekiti wa halmashauri ya mji.

Pia mwenyekiti huyo amesema kuwa baada ya watumishi wa halmashauri kupata taarifa ya kuondoka katika majengo hayo na kurudi katika makao makuu ya halmashauri yao yaliyoko  katika Kata ya Nyamilangano  badala ya kukabidhi majengo yakiwa na hali nzuri badala yake waliamua kupasua vioo vya madirisha huku nyaraka mbalimbali za ofisi zikionekana jambo ambalo ni hatari.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba alisema kuanzia 2014 majengo hayo yalikuwa yamekabidhiwa kwa halmashauri ya mji lakini Ushetu waliomba wakae kwa muda wakati ujenzi wa makao makuu huko Kata ya Nyamilangano unaendelea.

Hata hivyo kwa taarifa za kuaminika kutoka chanzo chetu cha habari wilayani hapa kimesema kuwa kufuatia halmashauri makabidhiano hayo ya makao makuu ya ofisi mjini Kahama baadhi ya Madiwani wa halmashauri ya Ushetu wamepanga kumgawana mkurugenzi mtendaji Michael Matomola na kutishia kumfungia ndani kutokana na amekabidhi majengo hayo bila kushirikisha baraza la Madiwani hao.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji Anderson Msumba akimwelekeza mwenyekiti wa halmashauri hiyo , Abel Shija majengo  waliyokabidhiwa na halmashauri ya Ushetu. 

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji akitoa maelekezo kwa mwenyekiti wa halmashauri ya mji abel Shija.

Ukumbi wa halmashauri ya mji kwaaji ya mikutano na vikao vya halmashauri ya mji ambapo tarehe 12 mwezi huu utatumika .

Muonekano wa majengo ya ofisi yaliyoachwa na halmashauri ya Ushetu na kukabidhiwa halmashauri ya Mji.

Friday, 7 April 2017

KICHANGA CHADAIWA KUTUPWA KWENYE DIMBWI LA MAJI TAKA SIKU MOJA.

Kichanga muda mfupi tu baada ya kuzaliwa na kutupwa kwenya maji machafu  kahama 

 Afisa maendeleo ya jamii  akionyesha kichanga baada ya kufikishwa katika hospital ya mji wa kahama 

Monge Mdeka (30) Ndiye mama wa kichanga hicho cha siku moja baada ya kukitupa kwenye shimo la maji taka


KAHAMA

 mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Monge Mdeka (30) mkazi wa kata ya zongomela katika halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga ametupa  mtoto wake wa siku moja kwenye dimbwi la maji taka.

Mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia Koplo Ninael Kisangase akizungumza na wandishi wa Habari alioambatana nao katika tukio hilo alielezea kusikitishwa na kitendo hicho cha kikatili kilichofanywa na mwanamke huyo na kudai kuwa wanawake waenzake wanaadhimisha siku yao yeye ameitumia kutupa mtoto kwenye maji machafu.

Aidha Koplo Kisangase aliwambia wandishi wa habari kuwa alipokea taarifa za kutupwa mtoto kutoka kwa wasamaria wema na wenyeuchungu na watoto wakati     walikwenda katika eneo la tukio nakukuta mtoto mchanga wa siku moja anaelea kwenye maji machafu ndani ya dimbwi lililoko eneo la kijiji cha Bukondamoyo Kata ya Zongomela.

Pia Koplo Kisangase alisema kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Kahama kwa uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha tukio hilo na akibainika kutenda kosa hilo kwa makusudi sheria 
 

MKURENGEZI WA MJI WA KAHAMA ATEKELEZA AGIZO LA DC HOSPITALI YA KAHAMA

 Mkurungezi wa Mji wa kahama Anderson Msumba
 
MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kahama mkoa wa Shinyanga Anderson Msumba amemuondoa kwenye nafasi yake ya kazi mhasibu wa hospitali ya mji huo, Mirian Mwakasenge kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha.

Mwakasenge pia anatuhumiwa kuihujumu hospitali hiyo kwa kuingiza dawa zake hospitalini humo na kasha kuwauzia wagonjwa dawa zake binafsi badala ya dawa za hospitalini.

Hatua hiyo ya Msumba ni utekelezaji wa agizo la mkuu wa wilaya hiyo Fadhil Nkurlu ambaye hivi karibuni aliuagiza uongozi wa hospiali hiyo kuwawajibisha watu wote waliohusika kufuja fedha za mapato ya hospitalini na kusababisha kupungua kwa mapato kutoka sh. milioni 45-20 kwa mwezi.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana Msumba alisema kuwa kutokana na agizo hilo la DC, uongozi wake ulifanya uchunguzi wa kina na kubaini chanzo ni mhasibu wa hospitali hiyo kuingiza dawa zake hospitalini na kuwauzia wagonjwa dawa zake binafsi.

“Hospitali ya mji inahudumia wagonjwa wengi sana na asilimia kubwa inahudumia wagonjwa wa halmashauri tatu za Ushetu, Msalala na Kahama mji pamoja na  wilaya jirani za Bukombe, Mbogwe, Nyang’hwale na Nzega lazima mapato yangekuwa juu lakini kwa sasa mapato yapo chini, hii inatokana na ubadhilifu unaazia kwenye uandikishaji wav yeti dirisha la malipo na inaonyesha Tehama inachengeshwa ili kufanyika kwa wizi,” alisema Msumba

ENEO LA MAZIKO MHONGOLO LAPATIWA UFUMBUZI KAHAMA

Mwenyekiti wa Halmashauri mji wa kahama Abel shija 

KUFUATIA mgogoro baina ya wananchi na ofisi ya kata ya Mhongolo wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, kuhusu eneo lililokuwa klimetengwa kwaajili ya huduma za kijamii na kuvamiwa na baadhi ya wananchi waliojenga makazi ya kuishi halmashauri ya mji huo imelipatia ufumbuzi.

Hali ya kupatikana kwa eneo hilo imekuja baada ya siku chache wananchi wa mtaa Mhongolo kwenda na jeneza katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata Maziku hiyo Mbusili na kulazimisha wazike mbele ya ofisi yake kwa madai wamekosa eneo la kuzika kutokana na eneo lao liliuzwa na diwani Michael Mizubo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama, Abel Shija aliyeongozana na wataalamu wa ardhi kutoka halmashauri huku wakiwa wamebeba lamani nzima ya kata hiyo walifika katika eneo la bega kwa bega naa kuonesha mipaka ya eneo hilo la maziko na kuwakabidhi wahusika ili waendelee kupata huduma hiyo muhimu.

Aidha mwenyekiti huyo wa halmashauri wakati akiwaonyesha mipaka wananchi hao aliwataka waanze mara moja kupata huduma hiyo huku akidai kuwa pamoja na ramani hiyo kubainika kuwa na mapungufu haiwazuii kupata huduma hiyo na kuwaagiza wataalamu hao wa ardhi kufanya maboresho ya ramani hiyo kwa kuongeza eneo la soko na uwanja wa mpira.

MWISHO 


Wednesday, 5 April 2017

SERIKALI KAHAMA WAPAA ONYO KALI WATUMISHI WA IDARA YA AFYA

 Mkuu wa wilaya ya kahama Fadhiri Nkurlu Wakati wa kikao kazi cha watumishi wa afya katika hospital ya mji wa kahama kwa baadhi ya watumishi wa idara hiyo kukosa maadili ya utumishi 

Watumishi wa afya wakisikiliza maelekezo ya kikao kazi toka kwa mkuu wa wilaya ya kahama Fadhiri Nkurlu mjin kahama  

 tumekuelewa mkuu  hayo ni baadhi ya maneno ya watumishi wa afya wa hospital mji wa kahma 

tuweke kumbumbkumbu sahihi 

baadhi ya watumishi  wa afya kama unavyoona maelekezo ya mkuu wa wilaya kama yatafanikiwa kwa hilo jambo

 Tuko makini 


 Baadhi ya madaktali wa hospital ya mji wakahama Dr masasi mwenye shati nyeupe na mwenye shati ya mabaka ni dr magesa 

KAHAMA

SERIKALI wilayani Kahama mkoani Shinyanga imewatahadharisha wauguzi wenye lugha chafu wakati wanapotoa hutuma za matibabu kwa wagonjwa wanaokwenda kutibiwa katika hospitali ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga.Tahadhal hiyo imetolewa leo na mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhil Nkurlu wakati akizungumza katika kikao baina yake na watumishi wa hospitali ya mji wa Kahama kilichofanyika katika ukumbi wa wauguzi.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa amekuwa akipokea malalamiko ya mara kwa mara juu ya manyanyaso wanayoyapata wakina mama wajawazito wanaofika katika wodi ya wazazi kwa lengo la kujifungua.

Aidha Nkurlu amesema kutokana na hali hiyo kuna umuhimu way eye kama kiongozi wa wilaya  ameona umuhimu wa yeye kujikita katika suala la afya ili wauguzi wawahudumie  kwa nidhamu wagonjwa wanaofika kwa lengo la kujifungua. 

Travel