Na Mohab Dominick
Kahama
May 21, 2014.
UMOJA wa Wazee Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga (UWAKA)
juzi ulikataa Mwaliko wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Kahama
kutokana kile wachosema kuwa mpaka Madiwani wanne ambao hawakwenda katika ziara
ya kujifunza katika Jiji la Mbeya kurudisha fedha za Wananchi walizochukua
kiasi cha Milioni 1.9 na kisha kukwepa safari hiyo
Katika barua yao kwa vyombo vya habari yenye kumb Namba
UWAKA/KHM/2014/43 kupitia kwa katibu wa umoja huo Paul Ntelya wazee hao
walikataa Mwaliko huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama
kuhudhuria kikao kwa pia ya Halmashauri hiyo haiutambui umoja huo.
Ntelya alisema kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Machibya
Judulamabambasi alitangaza kutoutambua umoja huo kupitia katika vyombo vya
Habari zikiwemo Radio Station hali ambayo walisema ni kama kitendo cha
kuwadhalilisha katika jamii.
“Hatuoni Mantinki ya kukubali Mwaliko huo labda kama
Mwenyewkiti wa Halmashauri ya Mji huo abadilishe uamuzi wake kupitia katika
vyomba vya habari vilevile kama alifanya
mwanzo ili dunia yote ipate kujua”, Alisema Paul Ntelya Katibu wa Umoja wa
Wazee Wilayani Kahama.
Ntelya alisema pamoja na kutokubali Mwaliko huo bado umoja
wa Wazee Wilayani hapa unasisitiza kuwa Madiwani Mabubu Musa Mabubu, James
Mlekwa, Bobson Wambura na Josephine Balanoga waliopewa fedha za posho kwa ajili
ya safari ya kwenda katika Jiji la Mbeya kujifunza na kutoenda wazirejeshe
fedha hizo katika muda wa suku 30 kinyume cha hapo umoja huo utawafikisha
mahakamani.
“fedha za Halmashauri ni Kodi za Wananchi na sisi Wazee moja
ya Wananchi na tuna uwezo wa kuhoji juu ya matumizi ya fedha za zinazotokana na
Walipakodi na hizo fedha walizotumia katika safari yao ya siku tano ni
kwetu”,Aliongeza Paul Ntelya Katibu wa Umoja wa Wazee Kahama.
Katibu huyo wa Wazee aliendelea kusema kuwa kitendo cha
Madiwani hao kuchukua posho kiasi cha shilingi 480,000 kila mmoja na kuhairisha
safari ni kama kitendo cha wizi cha kuwaibia Wananchi fedha zao za kodi
wanazochangia kwa Serikali.
Baadhi ya Madiwani walionekana wakinunua Mabati na vifaa
vingine vua ujenzi baada ya kuchukia kiasi hicho cha fedha hali ambayo baadhi
ya Wananchi walionekana kukerwa na kitendo hicho wakiwemo Wazee na hivyo
kufanya kuhoji juu ya Madiwani hao kukwepa safari hiyo na kubaki huku wangine
wakiishia katikati ya safari.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Machibya
Jidulamabambasi alipohojiwa juu ya suala hilo alisema Halmashauri yake bado
inalifanyia kazi suala hilo lakini kimsingi Madiwani wake hawawajibiki kwa
Wazee
Mwisho.
No comments: