UZINDUZI WA BARABARA: Rais Magufuli awasili Stendi ya Biharamulo

 RAI John Mpombe Magufuli  akifungua barabara ya Biharamulo 
Rais John Magufuli amewasili katika stendi ya Biharamulo mkoani Kagera ambapo unafanyika uzinduzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Kagoma- Biharamulo-Lusahunga.


Pamoja na uzinduzi Rais Magufuli pia atahutubia wananchi ambako umati mkubwa umehudhuria uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 154.

Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kanda ziwa, kanda ya kati na kanda ya magharibi.

Barabara hii inaunganisha mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Uganda na Rwanda .
 

UZINDUZI WA BARABARA: Rais Magufuli awasili Stendi ya Biharamulo UZINDUZI WA BARABARA: Rais Magufuli awasili Stendi ya Biharamulo Reviewed by Mohab Dominic on 22:26 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.