sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

WATAALAM WA MADINI YA DHAHABU NCHI ZA UKANDA WA MAZIWA MAKUU (ICGLR) WAKUTANA ARUSHA

Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wamekutana Jijini Arusha ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu madini hayo kwa maslahi mapana ya nchi hizo.

Mkutano huo wa siku mbili ulifunguliwa jana Machi 27, 2018 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambapo alisisitiza kuwa Nchi Wanachama wa ICGLR wanao wajibu wa pamoja kuhakikisha malengo waliyojiwekea yanafikiwa kwa manufaa ya wanachama wote.

Gambo alizungumzia changamoto mbalimbali zinazozikabili Nchi Wanachama ambazo ni uvunaji haramu wa madini, utoroshwaji wa madini, uharibifu wa mazingira, ukosefu wa teknolojia na baadhi ya Nchi kuwa na changamoto za Kiusalama.

Hata hivyo alisema changamoto hizo zisiwe sababu ya kurudi nyuma badala yake juhudi za pamoja, mshikamano wa dhati unahitajika ili kukabiliana na changamoto hizo na kuhakikisha ufumbuzi unapatikana kwa maslahi mapana ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.

Nchi Wanachama ni Tanzania, Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo (Kinshasa), Congo (Brazzaville), Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Sudan Kaskazini, Uganda na Zambia.

Tanzania imekuwa Mwanachama rasmi wa ICGLR Mwaka 2008 na tangu wakati huo imeendelea kutekeleza malengo ya mpango wa ICGLR ili kufanikisha udhibiti wa uvunaji haramu wa madini na kuhakikisha manufaa ya pamoja ya rasilimali husika yanapatikana.


 
 Baadhi ya Waratibu wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakifuatilia majadiliano kwenye mkutano huo Jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi wa Demokrasia na Utawala Bora- ICGLR, Balozi Ambeyi Ligabo akifuatiwa na Mwenyekiti wa Mkutano, Service Julie kutoka Congo

 Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na majadiliano.

 Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakifuatilia majadiliano

 Mwenyekiti wa mkutano, Service Julie kutoka Congo (wa pili kulia) akizungumza wakati wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR.

 Washiriki kutoka Tanzania wakifuatilia majadiliano kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Juma akimwakilisha Kamishna wa Madini, Prof. Shukran Manya na Mhandisi Fadhili Kitivai (kutoka Wizara ya Madini).

 Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na majadiliano Jijini Arusha.
 



Mwanaume Ajiua Kisa Penzi la Mkewe na Mchepuko..Aacha Ujumbe Huu Hapa


Mwanaume Ajiua Kisa Penzi la Mkewe na Mchepuko..Aacha Ujumbe Huu Hapa

Ujumbe wa Yona Kabla ya kifo chake....

"Nimekuwa kwenye matatizo ya ndoa kwa miaka 4, kila wiki nikipambana na mke mlevi na mzinzi.
Tukio la jana usiku na leo asubuhi limenisononesha na kunitia simanzi kubwa. Nimekata tamaa ya kila kitu na kila jambo nangoja mapenzi ya Mungu tu. Nalazimika kutumia dawa za usingizi lakini wapi. Sasa nipumzike nimwache mke wangu Eng Mloelya na mchepuko wake Eng Lossy wa Idara ya Maji Mbeya waendee!" Yona 

Hii Hapa Kauli ya Jokate kuhusu kugombea CCM


Hii Hapa Kauli ya Jokate kuhusu kugombea CCM

Mjasiriamali na Mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo amesema hana mpango wa kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Jokate ameiambia Clouds Fm kuwa anachofanya sasa hivi ndani ya chama hicho ni kuhamasisha ili kiweze kuwasaidia wananchi wa Kitanzania kwa ueledi na kwa usahihi.

“Tunajitolea kwa ajili ya chama naamini kuwa chama ndio serikali, kwa hiyo mimi nasaidia tu, naishia hapo, ni mapenzi wangu kwa vijana,” amesema.

Kuhusu kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani CCM, alijibu, “Sijui, haipo kwenye plan, haipo kwenye ramani yangu,”.

Kesi ya Agnes Masogange Yakwama

Kesi ya Agnes Masogange Yakwama

Upande wa mashtaka katika kesi ya  kutumia dawa za kulevya inayomkabili Agnes Gerald maarufu kama ‘Masogange’ umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwaonya  upande wa utetezi kwa kushindwa kutoa ushahidi  wao  kwa mara ya tatu mfululizo.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa wakili mwenzake, Reuben Simwanza ndiye aliyeandaa mashahidi na kwamba ameshindwa kutokea kwa kuwa anaumwa.

Wakili wa Serikali, Constantine Kakula alitaka upande huo uonywe leo Jumatano baada ya shauri hilo kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Kutokana na hali hiyo, Wakili Nkoko amesema atahakikisha anaandaa mashahidi ili itakapotokea wakili mmoja hayupo, mwengine aendelee na shauri.

"Hatuna pingamizi na sababu zilizotolewa na upande wa utetezi lakini tunaomba  Mahakama itambue kuwa ni mara ya tatu kwa upande wa utetezi inaahirishwa kesi hii? Amesema wakili wa Kakula na kuongeza;

"Mawakili wapo wengi lakini wanashindwa kuendelea kutoa ushahidi wao wa upande wa utetezi basi kama hawawezi, waache mshitakiwa aendelee na kesi mwenyewe."

Kutokana na hali hiyo, upande wa mashtaka umeomba ahirisho la mwisho kwa sababu kesi ni ya muda mrefu.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 26, mwaka huu  kwa ajili ya kusikilizwa.

Masogange ataanza kujitetea baada ya Mahakama kumkuta na kesi ya kujibu baada ya kusikiliza mashahidi watatu wa upande wa mashitaka. 

Baba Awapa Adhabu ya Ajabu Watoto Wake.

Baba Awapa Adhabu ya Ajabu Watoto Wake.

Mwanamume mmoja ametoroka nchini Burundi baada ya kuwapa adhabu ya kikatili watoto wake wawili ambao inadaiwa aliwapata wakiiba mahindi kwenye shamba lake.

Mwanaume huyo aliwazika ardhini wanawe wawili hadi sehemu ya vifua kabla ya kuwachapa viboko.

Walibahatika kuokolewa na mpita njia ambaye alikuwa jirani yao .

Kulingana na taarifa ya mwandishi wa BBC Prime Ndikumagenge kutoka Bujumbura.

Tukio hilo la ajabu lilitokea katika kijiji cha Bubanza, mkoa wa kaskazini magharibi mwa mji mkuu Bujumbura Jumapili jioni.

Taarifa zinasema watoto hao wenye umri kati ya miaka 8 na 10 walikamatwa wakiwa wanaiba katika shamba la mahindi.

Mmiliki wa shamba hilo aliamua kuchimba mashimo mawili na kumzika kila mmoja wao hadi usawa wa vifua vyao na kuanza kuwatandika viboko.

Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa hawajui ni nini kingetokea kwa watoto hao kama jirani yao asingepita.

Mwanaume huyo kisha alitoroka na watoto hao wakaokolewa.

Polisi wanasema bado wanamsaka mwanaume huyo kwa ajili ya kumfikisha mbele ya sheria.

Si mara ya kwanza kwa tukio la aina hii la kikatili dhidi ya watoto kufanyika nchini Burundi.

Watoto wawili walikatwa mikono yao ya kushoto katika jimbo la kati la Gitega mwezi Novemba mwaka jana baada ya kupatikana wakiiba mahindi

Moni Amfungukia Roma

Moni Amfungukia Roma


Msanii wa muziki wa Hip Hop, Moni Centrozone amedai kwamba Roma Mkatoliki hana mchango wowote katika maisha yake ya muziki kama watu wanavyofikiria.

Rapa huyo kutoka Dodoma, amesema kwamba hawezi kumzungumzia Roma kwa jinsi yoyote kwenye sanaa yake na hata kolabo watu wanayofikiria kuwa ilimpa msaada wa kumtambulisha wanakosea kwani haijam[patia lolote zaidi ya dhahama.

Majibu hayo ya ku-‘panick’ yaliyotolewa na Moni yallikuja baada ya kuulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho kama yeye na Country Boy wameamua kuanzisha muungano waliouita (MoCo) ili kushindana na muungano wa ROSTAM unaoundwa na Roma na Stamina na kudai yeye hashindani na watu hao bali yupo kwenye muziki kwa ajili ya kushindana na wasanii.

Moni ameendelea kusema mtu pekee ambaye anayemkumbuka na hawezi kumsahau katika sanaa yake miaka yake yote ni Marehemu Langa kwa kuwa ndo msanii ambaye aligundua kipaji chake na kumchukua kutoka kijijini kisha kumleta mjini kwa ajili ya kurikodi nyimbo na mapaka leo watu wanamtambua.

“Who is Roma kwenye maisha yangu. Mimi simfahamu na wala hajawahi kuntoa kwenye muziki kama jinsi watu wanavyoodhani. Mimi namjua Langa aliyenichukua uswahilini kwetu na kunileta mjini. Sipendi kutajiwa majina ya watu wasio na umuhimu na mimi” alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.

Mbali na hayo Moni amesema kwamba kundi lao MoCo’ haliwazuii kufanya nyimbo zao binafsi kama ‘solo artist’ na kusema kundi lao limewaunganisha ili kuweza kuleta changamoto kwa wasanii wote ambao wanafanya mziki sawa na wakwao na hawajamlenga kundi wala mtu yeyote.

Mapema mwaka jana Moni alimshirikisha Roma wimbo wake ambao ulimtambulisha zaidi kwenye ‘game’ ya Bongo kisha kumpatia mashabiki kibao na baadae mahusiano yao yakaonekana kuingia dosari pale mwezi Aprili wasanii hao walipotekwa na watu wasiojulikana kisha kuachiwa baada ya siku tatu na baada ya miezi kadhaa Roma akaachia wimbo aliouita ‘Zimbabwe’ ambao ulipata mapokeo makubwa na baadaye Moni kukasirika kwamba kwa nini Roma ameamua kutumia Idea ya kutekwa kwao na kufanya kama tukio hilo lilimtokea yeye binafsi na kumbe liliwapata watu wanne. (Roma, Moni

USILIE NADIA SEHEMU YA ISHILINI NA MOJA(21) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA ISHILINI(20) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA KUMI NA TISA(19) SIMULIZI YA KWELI



USILIE NADIA SEHEMU YA KUMI NA NANE(18) SIMULIZI YA KWELI



USILIE NADIA SEHEMU YA KUMI NA SABA(17) SIMULIZI YA KWELI



USILIE NADIA SEHEMU YA KUMI NA SITA(16) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA KUMI NA TANO(15) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA KUMI NA NNE(14) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA KUMI NA TATU(13) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA KUMI NA MBILI(12) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA KUMI NA MOJA(11) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA KUMI(10) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA TISA(9) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA NANE(8) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA SABA(7) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA SITA(6) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA TANO(5) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA NNE(4) SIMULIZI YA KWELI


USILIE NADIA SEHEMU YA TATU(3) SIMULIZI YA KWELI