Wataalam wa Madini ya Dhahabu
kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wamekutana Jijini Arusha ili
kujadili masuala mbalimbali yanayohusu madini hayo kwa maslahi mapana ya nchi
hizo.
Mkutano huo wa siku mbili
ulifunguliwa jana Machi 27, 2018 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambapo
alisisitiza kuwa Nchi Wanachama wa ICGLR wanao wajibu wa pamoja kuhakikisha
malengo waliyojiwekea yanafikiwa kwa manufaa ya wanachama wote.
Gambo alizungumzia changamoto
mbalimbali zinazozikabili Nchi Wanachama ambazo ni uvunaji haramu wa madini,
utoroshwaji wa madini, uharibifu wa mazingira, ukosefu wa teknolojia na baadhi
ya Nchi kuwa na changamoto za Kiusalama.
Hata hivyo alisema changamoto hizo zisiwe
sababu ya kurudi nyuma badala yake juhudi za pamoja, mshikamano wa dhati
unahitajika ili kukabiliana na changamoto hizo na kuhakikisha ufumbuzi
unapatikana kwa maslahi mapana ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Nchi Wanachama ni Tanzania, Angola,
Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo (Kinshasa), Congo (Brazzaville),
Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Sudan Kaskazini, Uganda na Zambia.
Tanzania imekuwa Mwanachama rasmi
wa ICGLR Mwaka 2008 na tangu wakati huo imeendelea kutekeleza malengo ya mpango
wa ICGLR ili kufanikisha udhibiti wa uvunaji haramu wa madini na kuhakikisha
manufaa ya pamoja ya rasilimali husika yanapatikana.
Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na majadiliano. |
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakifuatilia majadiliano |
Mwenyekiti wa mkutano, Service Julie kutoka Congo (wa pili kulia) akizungumza wakati wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR. |
Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na majadiliano Jijini Arusha. |
No comments: