sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » WAKULIMA TUMBAKU KAHAMA WAPEWA SOMO NA CRDB



Na Mohab Dominick
Kahama
May 6, 201.

WAKULIMA TUMBAKU KAHAMA WAPEWA SOMO NA CRDB

VYAMA vya Msingi vya Wakulima wa zao la Tumbaku Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga vimetakiwa kushirikiana na Taasisi za kifedha yakiwemo Mabenki ili waweze kupata mikopo kwa haraka itakayokuza mitaji yao ya biashara kurejesha kwa wakati ulipangwa.

Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa kitengo ya asasi ndogondogo za kifedha Raymond Urassa alitoa Wito huo wakati akitoa masaada wa Mifuko 100 ya Saruji yenye thamani ya shilingi milioni mbili  kwa chama cha msingi cha Tumbaku cha Kangeme Kaya ya ulowa kwa lengo ya kujenga wadi wa Wazazi na akinamama wajawazito katika kata hiyo.

Urassa alisema kuwa Benki ya CRDB kwa sasa imeanza kushirikiana na na vyma vya msingi hasa vile vya wakulima wa zao Tumbaku lengo la kurudisha kiasi kidogo cha sehemu ya faida wanayoipata benki hiyo  katika shughuli za kijamii kwa Wananchi.

Alisema kuwa ili vyma vya msingi viweze kuendelea lazima wakulima washirikiane na kuonyesha umoja wao hasa wakati wa kurudisha Madeni ya Pembejeo wanazozikopo katika taasisi mbalimbali za fedha hususani katika Mabenki.

Pia Meneja Mahusiano huyo aliwataka wakulima kuhakikisha kuwa wanakuwa mstari wa mbele katika kuwadhibiti wale ambao wamekuwa wakitorosha Pembejeo ili kukimbia madeni waliokopeshwa na vyma vya msingi katika eneo husika.

Nae Mgeni Rasmi katika makabidhiano hayo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Halamshauri ya Ushetu John Duttu alisema kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka na kuongeza kuwa kutokana na msaada huo ulitolewa na Benki ya CRDB Wananchi katika eneo hilo hawana budi kuhakikisha kuwa wanajenga kwa nguvu zao hadi kufilkia katika lenta hali ambayo Halmashauri ya Wilaya itamalizia  kwa kezeka jingo hilo.

Dr. Duttu aliwataka wakazi wa Ulowa kuhakikisha wanatumia vizuri misaada inayotolewa na Wafadhili mbalimbali kwa nia ya kuleta maendeleo hali ambayo itawafanya watu mbalimbali kuwa ni nia ya kusadia katika maeneo hayo hususani makampuni tumbaku, Asasi za Kibenki pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.

“Wakulima wa zao la Tumbaku nao wanafamilia zinazowategemea na kwa kupata wodi ya wawazi katika kata hiyo familia zao zitakuwa na afya njema na hata mikopo waliokopa wanaweza kuwa na nguvu ya kuirejesha kwa wakati ulioapangwa”, Alisema Dr. john Duttu katika hafla hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata Ulowa Paschal Mayengo alisema kuwa Msaada ulitolewa na Benki ya CRDB utasadia katika kukuza mahusiano mazuri na wakazi wa Kata hiyo na kuongeza kuwa kukamilika kwa Wodi hiyo katika Zahanati hiyo kutanudaisha jumla ya wakazi 25,000 kutoka katika eneo hilo.

MWISHO.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply