Afisa Uhamiaji wa wilaya ya kahama akichukuwa maelenzo kwa wahamiaji Haramu katika ofisi za uhamiaji wilayani kahama.
Baadhi ya wahamiaji haramu wakiwa chini ya ulinzi baada ya kutiwa baroni mjini kahama.
Wahamiaji harama wakiwa katika ofisi ya uhamiaji kwa mahojiano
Afisa uhamiaji wilaya ya kahamakamishina zakaria missana akiongea na vyombo vya habari mbali mbali ofisini kwake jana juu ya wahamiaji haramu.wanaongia katika wilaya ya kahama mkoa wa shinyanga .
Muandishi wa habari wa TBC Taifa ,Greyson kakuru akichukuwa taarifa kwa wahamiaji harama katika ofisi ya uhamiaji wilayani kahama.
Kamishina wa uhamiaji Zakaria missana akifanya mahojiano na baadhi ya wahamiaji haramu ofisi kwake.
Baadhi ya wahamiaji haramu wakiwa chini ya ulinzi katika ofisi za uhamiaji wilayani kahama mkoani shinyanga.
Kamishina wa Uhamiaji wilaya ya kahama Zakaria Missana akionyesha kidole moja ya wahamiaji haramu ofisini kwake.
KAHAMA.
KUANZIA
mwezi wa kwanza hadi mwezi nne 2015 idara ya uhamiaji wilayani kahama mkoani
shinyanga imefanikiwa kuwarudisha nchini mwao wahamiaji haramu 31 kutoka nchi
mbalimbali nchini walioingia nchin Tanzania bila kufuata utaratibu,sheria na
kanuni za kuingia nchi.
Hayo
yalibainishwa jana na Ofisa uhamiaji wa wilaya ya kahama Zakaria Missana wakati
alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwakwe, ambapo alisema kuwa
idara ya uhamiaji inafanya kazi kwa kuzingatia sheria na taaratibu za nchi.
Alisema
kuwa raia waliorudishwa nchi mwao walikuwa raia kutoka nchi mbalimbali,ambapo
nchi hizo ni nchi ya Congo alikuwa raia mmoja(1), Burundi walikuwa raia
22,Uganda walikuwa raia 2, huku Kenya walikuwa 3, pamoja na Rwanda walikuwa
raia 3.
“Tunafanya
kazi vema kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama bila
kuwasahau wananchi katika maeneo mbalimbali ya mji wa kahama na mkoani ili
kukamilisha shughuli nzima lawatu kuingia nchi kiholela bila kufuata utaratibu
ikiwa ni pamoja na kulikomesha zoezi la kuingia nchini Tanzania bila kuwa na
kibari” alisema Ofisa Missana.
Hata
hivyo Missana alisema kunabaadhi ya raia kutoa nchi ya Burundi na Rwanda
walifikishwa mahakamani kwakosa la kukaidi amri ya serikali yakutorudi nchini
mwao,ambapo Audresile ni raia wa nchi ya
Burundi alikamatwa tarehe 27,04 kwakosa lakuingia nchi bila kibari na kuweka
makazi huku akidanganya kuwa anatoka ngara.
Alisema
kuwa Ndaisenga Nuru ni raia wa nchi ya Rwanda alikamatwa kwa mara ya pili
Tarehe 25 mwezi 4 mwaka 2015 kwakosa la kuingia nchini na kuweka makazi bila kufuata
sheria,taaratibu na kanuni za kukaa nchini huku akidanganya kuwa ni raia kutoka
Kigoma wilaya ya kasulu.
Aidha
missana alisema kuwa idara ya uhamiaji imekuwa ikifanya kazi kwa ushirikiano na
wananchi ambapo Erick Venas Peter Raia wanchi ya Jamhuri ya Burundi alifukuzwa
nchini Tanzania kwakosa la kuingia nchini bila kibari hivyo na kukaidi amri ya
serikali ambapo aliendelea kuweka makazi, na alikamatwa na kufikishwa
mahakamani nakutozwa faini ya shilling 3000 au kwenda jela miezi 6.
Nae
Jokson Peter raia wanchi ya Burundi alikamatwa tarehe 27 mwezi 4 mwaka huu
nakufikishwa mahakama ya wilaya ya kahama kwakosa la kukaidi ya amri ya serikali
ya kuondoka nchi na kuhukumiwa kifungo cha kwenda jela miezi 30, ambapo missana
alisema jokson Peter alifukuzwa nchini 17/03/2009, hivyo nakukatwa 27/04/2015.
“Tumekuwa
tukifanya ukaguzi mara kwa mara katika maeneo mbalimbali,na tareh 4/05 mwaka
huu tulikagua katika gesti ya CDT na tulikuta wageni kutoka nchi
mbalimbali na walikuwa raia 27 katika gesti hiyo,hivyo basi Wakongo
walikuwa 10,waganda 2,Burundi 7,Rwanda 2 na Naigeria 1,nawageni wote walikuwa
na vibali halali vya kuingia na kutoka nchini” alisema ofisa Missana.
“Missana
aliendelea kusema kuwa”Sisi hatukatazi wageni kuingia nchini,bali sisi
tunawakataa wale wanaoingia kiholela bila kufuata utaratibu na sheria za
nchi,na tunatambua wazi kuwa kahama ni kitovu cha biashara na kahama napokea
wageni kutoka nchi za Rwanda,Kongo,Burundi,Ungada na Kenya na wote wanakuja
kuchua bidhaa kahama,sisi kama idara ya uhamiaji tunawaomba wafute sheria za
kuingia nchin”
.
Katika
hatua nyingine missana alisema kuwa kutokana na kauli ya jumuia ya afrika
mashariki imelenga kuhamasisha wanajumuia watembeleane kwa kufuata taaratibu za
uingiaji na utokaji wa nchi husika kwa kuwa na vibari halali na sio kutembelea
kiholela bila kufuata utaaratibu.
Mwisho
No comments: