KAHAMA
SIKU chache baada ya kutangazwa kwa
kura za maoni ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya kahama mkoani shinyanga
baadhi ya wanachama hicho katika kata ya kahama mjini wame kihama chama na
kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Akiongea blog hii mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na
maendeleo chadema wilaya Juma Protasi alisema kuwa jana wanachama zaidi
ya 50 wamejiunga na chama chake akiwemo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ushetu
Isaya Bukakiye pia ni mweka hazina wa wilaya ya kahama ambae ni miongoni mwa waliokabidhiwa kadi za chama.
Alisema kuwa miongoni mwa waliorudisha
kadi za chama cha mapinduzi ni pamoja na mabalozi 12 kutoka kahama
mjini,mwenyekiti wa CCM tawi la Majengo na wafuasi wengine wanaendelea kujiunga
na kutokana na mizengwe iliyotumika katika uchaguzi wa kura za maoni.
“Tumepokea mabalozi 12 na mwenyekiti wa
ccm tawi la majengo kutokana na wao kutoku tendewa haki katika kura za maoni
hasa wakati wa kumpisha mgombea ambao wao walikuwa wakimhitaji,ambapo walikuwa
wakipiga kura walikuta majina yao yameuzwa kwa watu wengine na kwajambo hilo
ndilo limepelekea wao kujiunga na Chadema” alisema Protasi.
Katikia hatua nyingine alisema kuwa
chama cham Chadema kinaendelea kuimalisha ngome zake na kuandaa mazingira ya
ushindi ndani ya majimbo yote matatu ambayo ni pamoja na Ushetu,Kahama mjini
pamoja na Msalala lakini pia ikiwa ni pamoja na kupokea wananchama wapya
wanaohama kutoka katika vyama vingine vya siasa.
Mwisho.
No comments: