Hapa
ni katika ukumbi wa Katemi Hotel uliopo Ngokolo Mitumbani mjini
Shinyanga ambako leo kumefanyika mkutano wa wadau wa habari mkoani
Shinyanga ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa
Shinyanga(Shinyanga Press Club-SPC) ikiwa ni agizo la Umoja wa Klabu za
waandishi wa habari nchini Tanzania(UPTC) lengo likiwa ni kujadili namna
wadau mbalimbali watakavyoshirikiana kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu
ujao wa rais,wabunge na madiwani unakuwa huru na wa haki.Kauli mbiu ya
mkutano huo ni "Uchaguzi huru na haki bila waandishi wa habari
kuzingatia maadili ni ndoto.Mgeni rasmi alikuwa kaimu katibu tawala mkoa
wa Shinyanga ndugu George Andrew kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Ally Nassoro Rufunga
Mgeni
rasmi alikuwa kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga ndugu George Andrew
kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akifungua
mkutano huo ambapo aliwasisitiza waandishi wa habari kuzingatia maadili
yao ikiwa ni pamoja na kuepuka kupendelea mgombea wala chama siasa
Kaimu
katibu tawala mkoa wa Shinyanga ndugu George Andrew kwa niaba ya mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga alipongeza pia kazi kubwa
inayofanywa na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga katika kuutangaza
mkoa huo na shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanyika mkoani humo
Mgeni rasmi alikuwa kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga ndugu George
Andrew kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga
aliwataka waandishi wa habari kutoandika habari za kupotosha jamii
lakini pia kuepuka kununuliwa.
Mgeni rasmi akiteta jambo na mwenyekiti wa Shinyanga Press Club
Wajumbe wa mkutano huo wakiwa ukumbini
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama
Malunde akitoa taarifa kuhusu klabu hiyo ambayo sasa ina wanachama
38,kati yao 18 wanatoka wilaya ya Shinyanga,19 wilaya ya Kahama na mmoja
kutoka wilaya ya Kishapu.Katika taarifa hiyo bwana Malunde
aliwakumbusha wandishi wa habari kuzingatia maadili katika kipindi hiki
muhimu cha uchaguzi na kuongeza kuwa waandishi wa habari wanatakiwa
kuhubiri amani kupitia kalamu zao.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama
Malunde aliwataka waandishi wa habari kuepuka habari za uchochezi na
kutojiingiza katika siasa na kushabikia vyama vya siasa
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akizungumza katika mkutano huo
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Wajumbe wa mkutano wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mkutano unaendelea
Katibu mtendaji wa Shinyanga Press Club akizungumza katika mkutano huo
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Wadau wakiwa ukumbini
Endelea kuangalia matukio katika picha hapa chini
Picha zote na Emmanuel Mpanda,Stephen Wang'anyi,Patrick Mabula na John Mponeja
No comments: