Polisi wanne waliokuwa doria wakati
wa uchaguzi juzi usiku, walijikuta wakionja machungu ya maji ya kuwasha,
baada ya kumwagiwa na wenzao wakati wakijaribu kuwatawanya wafuasi wa
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) waliokuwa wakisherehekea matokeo ya
udiwani.
Kufuatia tukio hilo katika Kata ya Makumbusho, Dar es Salaam, askari hao walijikuta mikononi mwa raia wakipatiwa msaada wa huduma ya kwanza kutokana na gari lao kumwagiwa maji ya kuwasha, kufuatia gari lililokuwa mbele yao kufyatuka pampu na kuanza kurusha maji hayo.
Tukio hilo lilitokea katika Mtaa wa Mwananyamala A, karibu na nyumba za makazi ya watu, wakati magari matano ya askari yakiwa nyuma ya gari lenye maji ya kuwasha, wakijaribu kutuliza ghasia za wananchi waliokuwa wakiandamana kushangilia ushindi wa diwani aliyeshinda, Harub Ally.
Wakizungumza na Nipashe, wananchi hao walisema tukio hilo lilitokea wakati polisi hao wakijaribu kurusha maji hayo ili kuwatawanya, lakini pampu hiyo ilifyatuka na kuwamwagikia askari wenzao.
Kufuatia tukio hilo, wananchi walianza kuwapa msaada wa mafuta ya kujipaka na maji kabla ya kuelekea hospitali.
“Hawa askari walikuwa wanatumwagia haya maji ili kutuliza ghasia, lakini jambo la ajabu maji yakawamwagikia wao. Ilibidi tuwe wema tuanze kuwasaidia kwani hali zao zingekuwa mbaya sana na kama siyo msaada wetu raia wangedhurika sana,” alisema Haroub Juma.
Askari hao baada ya kupatiwa msaada wa huduma ya kwanza, walichukuliwa na wenzao na kukimbizwa hospitali.
CCM, UKAWA WAPIGANA KWA MAWE.

Katika eneo la Mwananyamala kwa Kopa, wafuasi wa vyama vya Chadema na CCM walijikuta wakirushiana mawe kutokana na kutokubaliana kwa matokeo ya ushindi wa diwani wa CCM kata hiyo, Songoro Mnyonge.
Kufuatia matokeo hayo, wafuasi wa Chadema walichana matokeo hayo hali iliyowalazimu wafuasi wa CCM kuingilia kati na kuanza kushambuliana kwa maneno na kurushiana mawe.
Hali hiyo ambayo ilidumu kwa takribani nusu saa, iliwalazimisha wananchi kukimbia kukwepa vurugu hizo baada ya Jeshi la Polisi kuingilia kati.
WAFUASI WA UKAWA WATEMBEZEWA KICHAPO
Katika eneo la Chuo Kikuu Huria, Jeshi la Polisi liliwatembezea kichapo kwa wafuasi wa Ukawa waliofika kituoni hapo kudai matokeo kabla ya wakati wa kuyatangaza.
Wananchi hao ambao walifika kituoni hapo saa 8:00 mchana, walijikuta wakitimua mbio, baada Polisi kuwakimbiza na kukamata baadhi yao.
CHANZO: NIPASHE
No comments: