Na Mashirika ya Habari
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani,
Papa Francis, amemvaa mgombea urais wa Marekani Donald Trump, na kumwita sio
Mkristo.
Papa Francis ameyasema hayo wakati
akiwa kwenye ndege akirejea Vatican akitoka nchini Mexico baada ya kuongoza
ibada kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.
Trump alinukuliwa kuwa akiwa Rais wa
Marekani atajenga ukuta kwenye mpaka wanchi yake na Mexico ili kuzuia wahalifu
kuingia Marekani hususan wauza “unga”.
Pia Papa Francis hakufurahishwa na
kauli za mgombea huyo tajiri zinazoashiria ubaguzi ambapo Trump amewahi kunukuliwa
kisema, endapo atachaguliwa kuwa rais wa Marekani, Waislamu hawataruhusiwa
kuinia nchini humo.
Papa alisema “Yeyote anayefikiria
kujenga ukuta baina ya Mexico na Marekani huyo sio Mkristo.” Papa alisema.
Akijibu matamshi hayo ya Papa, Trump
ambaye alikjuwa akifanya kampeni zake huko South Carolina, aliiita kauli ya
Papa kuwa si ya haki na kumwita Papa kuwa ni “mshenga) wa serikali ya Mexico”
“Sibabaishwi na kauli za Papa, ni
lazima tuzuie wahamiaji haramu.” Alisema Trump akimjibu Papa. na kuongeza kuwa
Papa atatambua Ukristo wa Trump, pale Vatican itakaposhambuliwa na Wanamgambo
wa Kiislamu, ISIS
MWISHO
No comments: