sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » Iran yafanikiwa kuifanya jaribio roketi ya kubeba setilaiti

 Iran imefanikiwa kuifanyia jaribio roketi ambayo ina uwezo wa kupeleka setilaiti hadi mzingo wa dunia, siku moja baada ya Marekani kuiwekea vikwazo vipya kufuatia mpango wake ya kinyuklia.
Roketi hiyo ya Phoenix ilirushwa kutoka kituo kipya cha anga za juu kilicho Semnan kaskazini mwa Iran.
Marekani ililaani jaribio hilo na kulitaja kuwa kitendo cha uchokozi.
Ndilo jaribio la tano la roketi iliyoundwa nchini Iran tangu mwaka 2009.
Televisheni ya taifa nchini Iran inasema kuwa roketi hiyo itabeba setilaiti ya uzito wa kilo 250 hadi umbali wa kilomita 500 angani.
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani, anasema kuwa ikiwa itathibitishwa, jaribo hilo linaweza kukiuka maazimio ya baraza la Umoja wa Mataifa.
Iran iliapa kujibu vikwazo vipya viivyotangazwa na Marekani ambavyo vililenga makampuni 18 au watu ambao wameunga mkono programu za Makombora za Iran.
Vikwazo hivyo vipya vilitangazwa siku moja baada ya utawala wa Trump kusema kuwa Iran inatekeleza makubaliano ya mwaka 2015 ya kuachana na mpango wa kinyukia.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply