sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WAZIRI MKUU AAGIZA UJENZI WA HOSPITALI TUNDUMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Shule ya Misingi ya Mwaka katika mji mdogo wa  Tunduma.  Alikuwa  katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017. 



NA OWM, TUNDUMA
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma wilayani Momba kuanzisha mradi wa ujenzi wa hospitali.

Amesema sh. milioni 900 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Halmashauri kwa sasa zianze kutumika katika kuanzisha ujenzi wa hospitali hiyo.

Agizo hilo alilitoa jana jioni (Ijumaa, Julai 21, 2017) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma.

“Kwa kuwa afya ni jambo muhimu katika utekelezaji wa kauli mbiu ya Rais Dkt. John Magufuli ya Hapa Kazi Tu, hivyo naagiza fedha zilizotengwa kuanza ujenzi wa ofisi zitumike katika ujenzi wa hospitali.”

Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa halmashauri hiyo kuongezea sh. milioni 126 katika ujenzi huo. Fedha hizo zilitengwa  kwa ajili ya kuwafidia wamiliki wa eneo lililotengwa awali kwa ajili ya kujenga hospitali, ambapo aliwataka watafute eneo lisilohitaji fidia.

Pia, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) iandae ramani kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo na kuhusu suala la ujenzi wa ofisi Serikali italishughulikia.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo baada ya Mbunge wa jimbo la Tunduma, Mheshimiwa Frank Mwakajoka aliyeiomba kuiomba Serikali kuwajengea hospitali kwa kuwa halmashauri hiyo haina hospitali, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi pale wanapohitaji huduma hiyo.

Naye Mkuu wa wilaya hiyo, Bw. Juma Irando alitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili wilaya hiyo kuwa ni ukosefu wa hospitali ya wilaya, ukosefu wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na ofisi za Halmashauri.

Pia changamoto nyingine ni ubovu wa miundombinu ya barabara iliwemo ya Makamba-Ikana inayotakiwa kukarabatiwa inayounganisha ukanda wa juu na chini ili wananchi wa ukanda wa juu waweze kufika makao makuu ya wilaya.

 
Baadhi ya wananchi wa mji mdogo wa Tunduma  mkoani Songwe wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Uwanja wa Shule ya Misngi ya Mwaka Julai 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipokagua eneo la ujenzi wa jengo la pamoja la forodha kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia  katika mji mdogo wa Tunduma. Alikuwa  katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza ujumbe kutoka kwa Chifu Jubeki Chimpansya wa  Momba baada ya kusimikwa na wazee wa mila kuwa Chifu Simpanji katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye Uwanja wa Shule ya Misngi ya Mwaka katika mji mdogo wa Tunduma mkoani Songwe Julai 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  (kushoto kwake) wakitazama gari lililotengenezwa na  Adam Zachariah Kinyekie wakati alipowasili kwenye uwanja wa Shule ya Misngi ya Mwaka katika mji Mdogo wa Tunduma kuhutubia mkutano wa hadhara Julai 21, 2017. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya na Songwe, Erasto Zambi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  wa Ujenzi wa banio na mfereji wa maji wakati alipotembelea mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Makamba wilayani Momba Julai 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Dickson Mwandambila ambaye ni mlemavu baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye  Uwanja wa Shule ya Msingi ya Mwaka katika mji mdogo wa Tunduma.  Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017. KWA HISANI YA KHAFAN SAID 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply