headlines

    9:53

sponsor

sponsor

Slider

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » Uhuru Kenyatta atangazwa mshindi wa kura ya urais, Raila Odinga apinga
 Mohab Dominic

 Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imemtangaza rais Uhuru Kenyatta kama mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa urais uliofanyika siku ya Jumanne wiki hii.

Baada ya kuhakiki upya kwa fomu zinazoonesha matokeo zilizopewa jina la 34 A na 34 B kutoka maeneo bunge na vituo vya kupigia kura, Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amesema rais Kenyatta alipata kura Milioni 8.2  sawa na asilimia 54.2 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Raila Odinga aliyepata kura Milioni 6.7 sawa na asilimia 44.7.
Ushindi huu unamaana kuwa rais Kenyatta alipata asilimia 50 na kura moja, ya jumla ya kura zilizopigwa lakini pia asilimia 25 ya kura zote angalau katika kaunti 24 kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo.
Chebukati ameeeleza kuwa kati ya wapiga kura zaidi ya Milioni 19 waliojiadikisha kupiga kura, Wakenya takriban Milioni 15 walishiriiki katika Uchaguzi huo.
Ushindi wa Kenyatta umekataliwa na muungano wa upinzani NASA na kusema, kura za mgombea wake ziliibiwa na matokeo yalibadilishwa.
Kabla ya kutangazwa kwa mshindi, NASA walikutana na Makamishena wa IEBC na kueleza hoja zao ikiwa ni pamoja na kutaka wadau wote kuruhusiwa kuthathmini mfumo wa tume hiyo.
Hata hivyo, Mawakala wa Odinga ambao ni Musalia Mudavadi na James Orengo, wamesema madai yao hayajatatuliwa licha ya kuahidiwa na Tume hiyo mapema Ijumaa mchana.
“Pamoja na kwamba walikubali kushughulikia madai yetu, wamekataa kuyafanyia kazi, tunaodoka hapa Bomas,” amesema Mudavadi.
Katiba ya Kenya inaeleza kuwa, yeyote anayekataa matokeo anaweza kwenda Mahakamani lakini, NASA wameonesha kuwa huenda wasiende kulalamikia matokeo haya.
“Tunawaachia Wakenya waone kilichofanyika, imani yetu ipo kwa wakenya,” amesema Orengo.
Aidha, upinzani umewashtumu waangalizi wa Kimataifa na kusema kauli yao haikuwa sahihi kuhusu Uchaguzi huo.
“Mwangalizi wa Jumuiya ya Madola, rais wa zamani wa Ghana John Mahama, hana uhusiano mzuri na mgombea wetu kwa sababu ni mpinzani wa rais wa sasa Ghana ambaye ni mwandani wa mgombea wetu,” amesema Orengo.
"Hawa waangalizi walikimbilia uamuzi wa kusema kuwa Uchaguzi huu ulikuwa huru na haki, wangehakikiwa kwanza," ameongeza.
Kutangazwa kwa matokeo haya kumewahuzunisha wafuasi wa upinzani huku ikiwa ni furaha kwa wafuasi wa rais Kenyatta.
Hali ni ya wasiwasi katika ngome ya wafuasi wa upinzani hasa mjini Kisumu.

«
Next
PROFESA MBARAWA ATOA MWEZI MMOJA KWA WAFANYABIAASHARA JNIA
»
Previous
MAKANISA, MISIKITI 31 KUBOMOLEWA oads guzi kuanzia eneo la Ubungo, Kimara, Mb a misikiti hiyo wamej awa na simanzi kutokana na kukumbwa na bomoabomoa hiyo. TANESCO WAKATALIWA KUKATA UMEME Jana waandishi wetu walishuhudia baadhi ya wananchi wakiwakataza mafundi wa Tanesco kukata umeme kwenye baadhi ya nyumba ambazo zimewekewa alama X eneo la Kimara Stop Over, hata hivyo, hakuna aliyekuwa tayari kusema sababu za kufanya hivyo. Kanisa la Ufufuo na Uzima. MAKANISA YENYE ALAMA YA X Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima lililopo Ubungo Maji, ni miongoni mwa nyumba za ibada zilizowekewa alama ya X, hivyo kiongozi huyo kukutwa na dhahma nyingine. Kiongozi huyo amekuwa akikumbwa na matukio mengi huku akifikishwa polisi na mahakamani mara kadhaa. Katika uchunguzi wa gazeti hili, imebainika kuwa makanisa mengine yatakayokumbwa na bomoabomoa hiyo ni Kanisa la Anglikana Stop Over, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibamba, KKKT Usharika wa Mbezi Luis, Kanisa Katoliki Kimara litakalobomolewa nusu, Kanisa Katoliki la Mbezi Luis, The River Healing Ministry of Tanzania la Kibamba na Kanisa la Calvary Salvation lililopo Kibamba. Makanisa mengine ni Kanisa la TAG Rejoice Center la Mbezi, Kanisa la Kaprenan lililopo Kibamba, TAG – Suka, Pentekoste of Tanzania Kiluvya, Nayoth Church Kiluvya, KLPT la Bwawani, Kapernan Centre Mbezi, TAG Calvary Temple Mbezi Inn na GRC Mbezi Inn. Shehe Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum. MENGINE YAMEBOMOLEWA Katika uchunguzi wetu, baadhi ya makanisa yameshabomolewa kutii agizo la kubomoa kwa hiyari likiwemo la Moravian Kimara Stop Over na KKKT Kibamba. Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dk. Alex Malasusa, Jumamosi iliyopita alikwenda kuwafariji na kuwatia moyo waumini wa kanisa lake ambao wamepatwa na simanzi kutokana na uamuzi huo wa serikali. “Najua mna huzuni, majengo mengi yatabomolewa na serikali ili kupisha ujenzi wa barabara, kwa hili hamna budi kukubali na kuamini kuwa hiyo ni baraka kwa Mungu, zaidi kuweni na amani, ombeni baraka na kumshukuru Mungu,” alisema Dk. Malasusa. Kwa upande wake, Mchungaji wa KKKT Kibamba, Mshiu Wilness alisema kanisa limepokea agizo la kutakiwa kuhama na kubomoa jengo hilo na kwamba, tayari wameshapata eneo jingine ambalo wanatarajia kuhamia. “Tumepokea, tunatarajia kuondoka na tutavunja kama tulivyoelekezwa,” alisisitiza kiongozi huyo. Msikiti. MISIKITI NAYO YAKUMBWA Licha ya makanisa hayo, kuna misikiti itakayokumbwa na bomoabomoa hiyo ambayo ni Masjid Kilumbi Islamic Center – Kimara Mwisho, Dalul Mustafah wa Kimara Stop Over, Masjid Baitul Maamur, Masjid Jaaria, Al Masjid Nuur uliopo Kiluvya, Masjid Jaalia Gogan, Masjid Nuur Kibamba CCM na misikiti mingine mitatu ya Mbezi Inn, Mbezi Luis na Temboni. VIONGOZI WA DINI WANENA Wakizungumzia bomoabomoa hiyo, baadhi ya mashehe na wachungaji wametaharuki, wakisema wamepokea maagizo ya serikali ya kutakiwa kuvunja majengo yao huku wengine wakimuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwatazama kwa jicho la huruma. Imamu wa Msikiti wa Jamsjid Jaria wa Kiluvya, Haidary Masenga alisema waumini wameathirika kisaikolojia kwa kutojua msikiti huo utakakohamishiwa kwa kuwa hakuna eneo walilopata. “Wote tunataka maendeleo na sisi hatupingi, lakini tunaomba tutazamwe kwa jicho la huruma tuachwe tuendelee kuabudu hapa. Mpaka sasa hatujui chochote tunasubiri tu hatima ya serikali kama watavunja au la,” alisema Imamu Masenga. Imamu Msaidizi wa Msikiti wa Kilumbi Islamic Center, Halfan Malima alimuomba Rais Magufuli kuwahurumia kwa kuwapa eneo lingine la ibada kwa kuwa bado hawajapata. Mchungaji wa Kanisa la The River Healing Ministry of Tanzania, John Kyashama alisema anaunga mkono agizo la serikali la kubomoa nyumba, makanisa na misikiti ili kupisha upanuzi wa barabara. Kyashama alisema hana kinyongo na rais na anaunga mkono mipango ya maendeleo anayoifanya na anawashauri wachungaji wenzake waliokumbwa na bomoabomoa kukubaliana na hali hiyo kwa kuwa kinachofanywa na serikali ni kwa nia njema. “Si vizuri kuwa na kinyongo wala kuzozana na utawala, kila mtu atii mamlaka za nchi,” aliasa mchungaji huyo. MALALAMIKO YA WANANCHI Licha ya nyumba hizo za ibada, baadhi ya majengo ya wananchi pia yamewekwa alama ya X ambapo wengi wameitupia lawama serikali kwa madai kwamba wakati wanajenga nyumba hizo, walikuwa hawajavunja sheria yoyote. Mzee John Mlangi (74), mkazi wa Kimara Stop Over alisema amejenga nyumba yake miaka 35 iliyopita na wakati huo hakukuwa na sheria ya ardhi aliyoivunja kwa kuwa alikuwa nje ya mita 60 kutoka kwenye barabara na kiwanja hicho alikuwa akikilipia kodi kwa miaka yote hiyo. “Kutokana na kuwekewa alama ya X nimekuwa nikiishi kwa wasiwasi na nimepata ugonjwa wa shinikizo la damu,” alisema. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Stop Over, Kimara, Magreth Msabuso alisema katika mtaa wake, wapo wazee wengi waliostaafu ambao ikiwa nyumba zao zitabomolewa bila fidia, hali zao zitakuwa mbaya. Alisema wananchi wote waliowekewa alama za X nyumba zao walipaswa kushirikishwa tangu hatua ya kwanza kabla ya kuweka alama hizo. POLISI NAO WAKUMBWA Mbali na nyumba hizo za kiraia na za kidini, pia Kituo cha Polisi Mbezi Luis kitabomolewa huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Muliro Jumanne akisema kilijengwa kwa nguvu za wananchi kutokana na mahitaji ya eneo hilo. Alisema kutokana na kuwekwa alama ya X, kituo hicho kitahamishiwa eneo la Gogoni kwa kuwa licha ya kuwa barabarani, bado eneo lake ni dogo. “Kituo hiki kitaondolewa hapa na kupelekwa kwenye kituo kingine cha Gogoni kilichojengwa chini ya mradi wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na ujenzi wake umeshirikisha nguvu za wananchi na ni kikubwa kwa Wilaya ya Ubungo,” alisema. VITUO VYA MAFUTA NAVYO BALAA Vituo vya mafuta navyo vimekumbwa na balaa hilo na vilivyowekewa alama ya X kwa ajili ya kubomolewa ni Camel Oil-Kimara Stop Over, Henry Filling Station-Mbezi kwa Yusuph, Camel Oil – Kibamba, Uduru Oil Station – Kibamba na Total-Stop Over. HUDUMA ZA AFYA ZAKUMBWA Vipo pia vituo vya huduma za afya vitakavyoguswa na bomoabomoa hiyo ambavyo ni Hospitali ya Boch na Kituo cha Afya cha Kimara vitakavyobomolewa nusu, Hospitali ya Neema iliyopo Kimara Stop Over, Kimara Centre Dispensary na Zahanati ya Arafa. Share: Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Related Posts: HATIMAE RUBANI MTANZANIA AHACHIWA HURU ZITTO NA SERIKALI VUTA NI KUVUTE UHABA WA CHAKULA NCHINI TAFITI- HII NDIO IDADI YA WATU WALIOUWAWA KATIKA AJALI ZA BARABARANI WAKURUGENZI TANESCO WASIMAMISHWA KAZI POLISI KUFUKUWA KABURI LA BINTI ALIZIKWA KWA SIRI ARUSHA ← Newer Post Older Post → Home 0 comments: Post a Comment Search Popular Tags Blog Archives HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE JANUARY 31 2017 Leo January 31 2017 Baraza la mitihani Tanzania ‘NECTA’ limetangaza matokeo ya k... TFF AIWATAMBUI OKWI, AJIBU Mshambuliaji wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu. Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limezikumbusha klabu zote ambazo zinasimamiwa na sh... MO AIGUSA PABAYA YANGA Bilionea wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’. HAKIKA vita ya wakubwa watoto wanatakiwa kukaa mbali, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya ... YANGA WAACHWA SOLEMBA Licha ya kuwa winga Ramadhani Singano alikuwa akiwania na Yanga ambapo tayari mazungumzo yalikuwa yameshafanyika ili asaini kikosini ha... OMOG AWANYIMA RAHA YANGA Kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima. TAARIFA za ujio wa kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima ndani ya Simba zimemkosha kocha wa timu h... BOKO NA SIMBA HII KAZI IPO MAZOEZINI Kikosi cha Simba kimetimiza wiki moja na ushei sasa kambini Afrika Kusini, lakini utamu umezidi kunoga baada . . ARA
Pages 22123456 »

No comments:

Leave a Reply