sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » BARRICK BUZWAGI YATUMIA MILIONI 43 KWA MWAKA KUSADIA WANAFUNZI WASIOKUWA NA UWEZO KATIKA SHULE TATU WILAYANI KAHAMA

MENEJA WA MGODI WA BUZWAGI FILBERT RWEYEMAMU AKIMKABIDHI MOJA WA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MWENDAKULIMA SALE ZA SHULE
Kahama
Jan 16, 2013.

BARRICK BUZWAGI YATUMIA MILIONI 43 KWA MWAKA KUSADIA WANAFUNZI WASIOKUWA NA UWEZO KATIKA SHULE TATU WILAYANI KAHAMA

KAMPUNI ya Afican Barrick kupitia Mgodi wake wa Buzwagi imetumia kiasi cha shilingi milioni 43.6 katika  kusadia Wanafunzi wasiokuwa na uwezo vifaa mbalimbali vya masomo katika shule tatu za sekondari zinazozunguka Mgodi huo ikiwa ni sambamba na kuwalipia karo za masomo kwa kipindi  mwaka 2013.

Kampuni hiyo kwa kupitia mradi wake wa Can Educate ambao wafanyakazi wa migodi yake huchangia kwa lengo la kusadia Wanafunzi tayari imekwishatoa msaada huo katika sekondari za Mwendakulima, Bugisha, pamoja na Sekondari ya Nyasubi ambazo zipo jirani na Mgodi huo.

Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo kwa awamu ya mwisho mjini Kahama kwa wanafunzi wa sekondaro hizo Meneja Mahusiano wa Mgodi huo huo Steve Kisakye alisema kuwa lengo la la Mgodi huo kusadia wanafunzi hao ni katika nia ya kuboesha Elimu kwa wanafunzi.

Kisakye aliendelea kusema kuwa lengo jingine ni katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata Elimu na kuongeza kuwa sio walio kando ya Mgodi wa Buzwagi tu ilahata wale waliopo jirani na migodi ya North Mara pamoja na Mgodi wa Tulawaka na Bulyanhulu.

Aidha Meneja mahusiano huyo alisema kuwa katika Mgodi wa Bulyanhulu wamesadia jumla ya wanafunzi 900, Mgodi wa North Mara Wanafunzi 200 wakati katika mgodi wa Buzwagi wamesadia wanafunzi 400 sambamba na ukarabatio wa shule ununuzi wa madawati, na Elimu ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wanaofanya vizuri.

Kwa upande wake Meneja Mgodi wa Buzwagi Filbert Rweyemamu alisema kuwa mgodi huo hautaacha kuwasadia wanafunzi  hao hasa wasijiweza katika kutimiza ndoto zao za baadaye ni hivyo kupata wasomi watakaoendesha migodi hiyo hapo siku za baadaye.

Rweyemamu alisema kuwa pia kwa kugawa misaada hiyo itakuwa ni changamoto kwa wanafunzi kufanya vizuri darasani na hata kupunguza kwa kiasi Fulani suala la utoro kama lilikuwepo kwa  wanafunzi kwa kuwa wana nyenzo za kusomea kwa sasa.

Akitoa Shukrani kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Richard Msagati aliwataka wawekezaji hao kutokata tama katika kusadia jamii ya kitanzania kwani kwa mgodi kuwa karibu  imekuwa msaada mkubwa kwao na kwa Halmashauri kwa ujumla.

Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi kupitia mradi huo wa Can Educate imeshasaidia mambo mbalimbali ya kielimu katika shule hizo kwa mwaka huu kama vile sale za shule kwa wanafunzi, sweta, kwa wanafunzi 400 huku wasichana wakiwa 185 na wavuala 215 ikiwa ni sambamba na karo za shule milioni nne Mwendakulima sekondari, milioni mbili Bugisha Sekondari na Nyasubi milioni mbili huku jumla ikiwa ni shilingi milioni nane huku kwa mwaka wakitoa jumla ya shilingi milioni 43.

Mwisho.

 BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE ZA MWENDAKULIMA ,NYASUBI.NA BUNGISI WAMSIKILIZA MENEJA WA MGODI WA DHAHABU WA BUZWAGI JANA MJINI KAHAMA
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MWENDAKULIMA WAKISOMA RISALA KWA MGENI RASMI WA MGODI WA DHAHABU WA BUZWAGI  MJINI KAHAMA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply