Kahama
Jan 22, 2014.
FANYENI KAZI KWA MAHUSIANO NA SII MALUMBANO; MENEJA
TRA MKOA WA SHINYANGA ERNEST MDEE
WAFANYABIASHARA Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
wametakiwa kufanyakazi kwa maelewano na ushirikiano na Mamlaka ya Mapato (TRA) Wilayani
hapa kwa lengo la kukuza mahusiano
mazuri baina ya Mlipa kodi na Mtoa kodi.
Hayo yalisemwa juzi na Meneja wa Mamlaka ya Mapato
Mkoa wa Shinyanga Ernest Mdee katika kikao kilichojumuisha Wafanyabiashara
kutoka katika sekta za Kilimo na Viwanda kilichofanyika mjini hapa.
Mdee alisema kuwa mfumo wa kulipa kodi ni rasilimali
katika nchi tena zinazoendelea na kuongeza kuwa kama wanyabiashara wataweza
kulipa kodi kwa muda muafaka kasi kungekuwa hakuna malumbano baina ya pande
hizo mbili.
Alisema kuwa kama kuna mambo ambayo wafanyabiashara
hawayaelewi katika mfumo mzima wa biashara zao basi Mamlaka yake ipo tayari
kutoa mafunzo kwa ajili ya kuwawezesha kwa urahisi na unafuu zaidi ili waweze
kufanya biashara zao vizuri.
Pia Meneja huyo aliwataka Wafanyabiashara kuwa na
moyo wa ujaili katika kuwataja majirani zao wanaokwepa kulipa kodi huku wakidai
kuwa mauzo yao ni madogo wakati mizigo wanayoshusha katika maduka yao ni
mikubwa kuliko kabadirio ya awali..
Kuhusu malalamiko ya Wafanyabiashara kuhusu mashine
mpya za kutoa risiti Meneja wa TRA Wilaya ya Kahama Peter Nkwabi alisema kuwa mashine hizo nzuri na kuongeza
kuwa kama kuna matatizo juu ya mashine hizo wafike katika ofisi husika ili
waweze kupata maelekezo zaidi.
Nkwabi aliwataka Wafanyabiashara kuwa na ushirikiano
katika mambo mbalimbali na Mamlaka yake na kuongea katika vikao vya pembeni
halia mbayo haitakuwa msaada kwa wafanyabiashara hao.
”Jamani Wafanyabiashara wa Kahama kama kuna matatizo baina ya maafisa wangu na
nyinyi ni bora matatizo hayo tukayazungumza na kuyamaliza na sii kuyazungumza
pembeni hali hii haita wasaidia”,Alisema Peter Nkwabi.
Awali kulikuwa na malalamiko baina ya
Wafanyabiashara wa Kahama kuwa Maafisa wa TRA wamekuwa wakipita katika maduka
yao kwa lengo la kufungua droo zao za fedha na kuwalazimisha kuhesabu fedha zao
ilikuona mauzo yao kwa siku hali ambayo wawalikuwa wakiilalamikia.
Wafanyabiashara Wilayani Kahama wamekuwa wakikwepa
kulipa kodi za serikali mara kwa mara hali ambayo maafisa wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania wakifika katika biashara za o wamekuwa wagumu katika kusema mauzo yao
wanayouza kwa siku na hivyo kuwafanya Maafisa wa TRA kukaa katika maduka yao
kwa siku nzima ili kuona na hivyo kuwafanya kuona kuwa wanaonewa.
MENEJA WA MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA SHINYANGA (TRA)ERNEST MDEE AKIONGEA NA WAFANYABIASHARA WA WILAYA YA KAHAMA JUU YA MATUMIZI YA MASHINE ZA( EFD)MJINI KAHAMA JANA
MWENYEKITI WA TCCIA WILAYA YA KAHAMA MEJA MSTAAF MATALA AKIWA NA MUANDISHI WA GAZETI LA HABARILEO MJINI KAHAMA RAYMOND MIHAYO KABLA YA KIKAO CHA WAFANYABIASHARA NA MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA SHINYANGA NA KAHAMA JUU YA MASHINE ZA (EFD )JANA MJINI HAPA
BAADHI YA WAFANYABIASHARA WA MJI WA KAHAMA KABLA KUANZA KIKAO KATIKA UKUMBI WA NITESHI JUU YA MASUALA HULIPAJI WA KODI NA MASHINE ZA( EFD)
MENEJA WA TRA MKOA WA SHINYANGA ERNEST MDEE AKITOA MAELEZO KWA WAFANYABIASHARA JUU YA ULIPAJI WA KODI YA MAPATO WILAYANI KAHAMA JANA
MENEJA WA MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA SHINYANGA AKIONYESHA WAFANYABIASHARA MASHINE YA( EFD) JINSI ILIVYO JANA KATIKA UKUMBI WA NITESHE JUU YA MATUMIZI ZA MASHINE HIZO
WAFANYABIASHARA WA WILAYA KAHAMA MAHOLELO MASUKA, WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MENEJA WA MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA SHINYANGA ERNEST MDEE ,JANA KATIKA KIKAO CHA KUFAHAMISHANA JUU YA MASHINE ZA( EFD)
No comments: