Na Mohab Dominick
Geita
Nov
11, 2013.
Rais jakaya mrisho kikwete Akihutubia wakazi wa uyovu wilayani Bukombe katika unziduzi wa barabara ya uyovu Bwanga yenye urefu wa kilometa 45 kwa kiwango cha lami picha na mohab Dominick.
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kama
kuna mtu jamii ya wafugaji ambaye ng’ombe zake zimepigwa Risasi na Askari wa
wanyamapori katika operesheni serikali kali haitasita kuwachulia hatua
wahusika.
Rais
Kikwete aliyasema hayo wakati akiwahutubia wakazi wa Mji wa Ushirimbo katika
mkutano wa hadhara juzi wakati wa ziara yake inayoendelea ya kukagua shughuli
mbalimbali za maendeleo katika Mkoa wa Geita.
Alisema
kuwa kwa sasa Kiwango cha uwindaji wa wanyapori kimefikia kiwango cha kutisha
hali ambyo Serikali haiwezi kuvumia uharamia huo na kuongeza kuwa katika
hifadhi sio mahali pa kulishia Ng’ombe bali na mahali pa kulishia wanyama pori.
“Nasema
kama kuna mfugaji ambaye ng’ombe zake zimepigwa Risasi na Askari wetu wa
Wanayamapori na ana ushahdi na uhakika wa kufanyika kwa vitendo hivyo basi
Serikali haitasita kuwachulia hatua Askari waliohusika”, Alisema Rais Kikwete.
Pamoja
na Mambo mengine katika hutuba yake hiyo Rais Kikwete alitoa tahadhari juu ya
ongezeko la maambukizo ya Ugonjwa hatari wa Ukimwi katika Wilaya ya Bukombe
kwani hadi kufikia sasa maambukizo hayo katika Wilaya hiyo yamefikia asilimia
6.3 kuzidi ile ya kitaifa ambayo ni 5.1.
Aidha
aliendelea kusema kuwa jumla ya watu 8,100 katika Wilaya hiyo wanaishi na
Virusi vya ukimwi huku watu 5,100 ndio
wanaotumia vidonge vya kurefusha maisha (ARV) na kuongeza kuwa sehemu
zinazoongoza kwa maambukizo ni pamoja na sehemu zenye machimbo madogomadogo.
Alizitaja
sehemu hizo kuwa ni pamoja na Katente, Kerezia pamoja na uyovu na kuongeza kuwa
watu hawana budi kubadilika na kuwasikiliza mawaidha kutoka kwa viongozi wa
dini juu ya tahadhari ya ugonjwa huo ambao umekuwa tishio hapo nchini.
Hata
hivyo alisema kuwa ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo lazima watu
wabadilike na kuwa waaminifu kwa wapenzi wao ikiwa ni sambamba na kutumia kinga
wakati wa kufanya kitendo hicho.
mwisho
No comments: