Na Mohab Dominick
Geita
Nov 11, 2013.
RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE MWENYE MIWANI NYEUSI KATI WA KWANZA KUSHOTO NI MILIKI WA MGODI HUO EMMANUEL GUNGU NA WAKWANZA KULIA NI NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI STEPHEN MASELE NA MWISHO NI NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI MAJALIWA MAJALIWA AKIWA NA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA JANA WILAYANI BUKOMBE MKOANI GEITA KATIKA ZIARA YAKE YA SIKU YA PILI MKOANI HAPA.
SEREKALI imesema kuwa haitaacha kuwasaidia
Wachimbaji wadogowadogo katika mambo mbalimbali ikiwemo kuwapatia Leseni za
Uchimbaji sambamba na maeneo ya kuchimbia ikiwa watafuata taratibu za kisheria
katika kufanya shughuli hizo kihalali.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya
Mrisho Kikwete aliyasema hayo wakati akifungua Mgodi mdogo wa Nsagali Gold Mine
(NGM) unaomilikiwa na mwekezaji mzawa kutoka hapa nchini Emanuel Gungu katika
mji wa Ushirombo juzi.
Rais Kikwete alisema kuwa Serikali haitaacha
kumsaidia mchimbaji mdogo hasa katika kumpatia mitambo mbalimbali kwa
ajili kufanya shughuli hizo uchimbaji
hali ambyo itamfanya mchimbaji mdogo naye kufanya kazi yake kwa uhuru
zaidi.
Katika taarifa ya ujenzi wa Mgodi huo iliyosomwa na
Mmoja wa wakurugenzi wake Njalu Silanga alisema kuwa Mgodi huo utanunua mchanga
wa marudio kutoka kwa wachimbaji wadogo na hivyo kuurudia kwa mara ya pili
kitaalamu ili kupata mali iliyomo.
Silanga alisema kuwa kutokana na ujenzi wa Mgodi huo
jumla ya watu 800 wamenufaika katika kupata ajira huku akiongeza kuwa watakuwa
wakizalisha kiasi cha tani 120 za mawe zitakuwa zikisagwa kwa siku katika Mgodi
huo.
Aidha aliendelea kusema kuwa Mgodi huo umegharimu
kiasi cha dola za kimarekani 251 sawa na
shilingi Bilioni 3.3 za kitanzania na kuongeza kuwa Kampuni yake mpaka kufikia
hivi sasa tayari imekwishaanza kusadia mambo mablimbali katika sekta za Elimu,
Maji na Afya katika aeneo la Katente mahali uliopo.
Hata hivyo Silanga alisema kuwa katika kuhakikisha
Mgodi huo mpya unawanufaisha wakazi wa mji wa Ushirombo alisema kuwa
wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa umeme hali ambyo inafanya
uzalishaji kuwa mdogo kwani wanatumia majenereta.
Katika ziara yake hiyo Mkoani Geita Rais Kikwete pia
aliambatana na baadhi ya Mawaziri akiwemo Waziri wa ujenzi John Magufuli,
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Stephen Masele, Naibu Waziro Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi Majaliwa Majali
pamoja na maafisa mbalimbali wa Serikali.
mwisho
No comments: