MADIWANI MJI KAHAMA WAMKATAA MGANGA MKUU WA
HOSPITALI YA WILAYA
Na Mohab Dominic
Kahama
May 22, 2014.
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Kahama juzi
lilimkataa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri hiyo Helen Membe kwa kile
walichesema kuwa hana sifa za kuongoza Madaktari wenye sifa na watumishi
wanaohudumia Wagonjwa katika Hospitali hiyo
.
Diwani wa Kata ya Majengo Bobson Wambura alisema kuwa Mganga
Mkuu huyo amepewa wadhifa huo huku akiwa hana sifa hata moja ya kuwa na cheo
hicho hali ambayo imefanya kuwepo na makundi ya Wafanyakazi wa Hospitali hiyo
pamoja na Waganga.
Alisema kuwa kutokana na Dr, Huyo Helen Membe kutokuwa na
sifa za kuongoza watumishi wa Hospitali hiyo pia kumesababisha kuwepo kwa
migomo baridi ya Madaktari hali ambayo imefanya Wagonjwa kutopata huduma kwa
wakati muafaka.
Kwa sasa Mheshimiwa Mwenyekiti kumekuwa na makundi
makubwa katika Hospitali hiyo kuanzia
Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wengine huku wakisema ni vigezo gani
vimepelekea Daktari huyo kupata wadhifa huo mkubwa”, Alihoji Bobson Wambura
Diwani wa Kata ya Majengo.
Aliendelea kusema kuwa kuhusu Mganga Mkuu huyo ni bora
Wizara ikiwa wazi juu ya Mtumishi huyo kwani ni mzigo na hana uwezo kuliko wale
waliopo chini yake hali ambayo imezua migogoro mingi isiyoisha katika Hospitali
hiyo baina ya Wafanyakazi na kiongozi huyo.
Diwani huyo aliendelea kusema katika Baraza hilo kuwa kwa
sasa katika Hospitali ya Wilaya baadhi ya Madaktari wamekuwa wakifanya kazi
katika Hospitali binafsi za watu huku wakiwaacha wagonjwa wakipata taabu ya
kutafuta huduma ya tiba katika Hospitali hiyo ya Wilaya.
“Ukienda sasa Hivi katika Hospitali ya Wilaya kutafuta
huduma huwezi kupata kwani madaktari wanafanya kazi katika Hospitali za Watu
binafsi na Wagonjwa wanabaki bila ya kuhudumiwa na inashangaza sana tunaomba
kiongozi huyo abadilishwe kwani kuna watu wenye sifa ya kuwa cheo hicho kuliko
daktari huyo”, Alisema Diwani huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama
Felix Kimaryo akijibu hoja hiyo aloisema
kuwa suala hilo limeishafika katika Ofisi yake na linashughulikiwa ipasavyo ili
kuhakkikisha wananchi kero inaondoka haraka iwezekanavyo katika Hospitali hiyo
ya Wilaya.
“Ndugu zangu Madiwani subirini masuala yanayohusu Hospitali
ya Wilaya yanashughulikiwa kwa mujibu wa kufuata sheria na taratibu na sii
lazima kusema hatua zinazochukuliwa na Halmashauri juu ya Mtumishi huyo mbele
Baraza zima la Madiwani kwani kikao hiki ni cha wazi”, Alisema Felix Kimaryo
Mkurugenzi wa Halmashuri ya Mji.
mwisho
No comments: