Na Mohab Dominick
Kahama
May 23, 2014.
2508 WAJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA JANA KAHAMA
JUMLA ya Wanafunzi wapatao 2508 waliomaliza darasa
la saba mwaka jana wamejiunga na kidato cha kwa kwanza katika shule mbalimbali
za binafsi na za Serikali Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ikiwa ni sawa na
asilimia 86 ya Wanafunzi wote waliofanya mtihani.
Hayo yalisemwa juzi na Afisa Elimu Sekondari wa
Halmashauri ya Mji wa Kahama Anastazia Manumbu katika baraza la Madiwani la
Halmashauri hiyo lililofanyika juzi Mjini Kahama na kuongeza kiwango
kilichokuwa kimepngiwa kwa ni Wanafunzi 2931.
Manumbu aliesema kuwa katika idadi hiyo ya Wanafunzi
waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba kwa mwaka jana 2013 wanawake 1331
huku wale wakiume wakiwa idadi ya Wanafunzi 1600.
Afisa Elimu huyo aliendelea kusema kuwa jumla ya
Wanafunzi 547 walijiunga katika shule za sekondari na Binafsi wakati idadi ya
Wanafunzi 1963 walijiunga katika Shule za sekondari za Serikali na hivyo
kutimia idadi hiyo ya Wanfunzi 2508.
Akielezea kwa upande wa shule za shule za Sekondari
Afisa Elimu huyo Manumbu alisema kuwa kiwango cha ufaulu kwa Wanafunzi wa
kidato cha nne kwa mwaka jana kimeongezeka kwa asilimia 74 ukilinganisha na
miaka ya nyuma.
Akizungumzia kuhusu mikakati ya Mkoa ya Mkoa wa
Shinyanga kwa Wilaya ya Kahama katika kukuza Elimu ya Sekondari Manumbu
aliesema kuwa mkoa umejipanga kwa kuweka mitihani ya utimilifu pamoja na ile ya
pamoja pamoja na mitihani ya mwisho.
Hata hivyo aliendelea kusema kuwa gharama za
mitihani hiyo itanchangiwa na Wazazi wa Wanafunzi huku kiwango cha mitihani
hiyo kikiwa jumla ya shilingi 10,000 kwa kila mwanafunzi atakayewajibika
kufanya mitihani hiyo,
mwisho
No comments: