sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » MGEJA; KAULI YA LEMBELI CCM SIO MAMA YAKE NI KUVIMBIWA MADARAKANa  Mohab Dominick
Kahama
May 6, 2014.

MGEJA; KAULI YA LEMBELI CCM SIO MAMA YAKE NI KUVIMBIWA MADARAKA

CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga kimesema kuwa kauli ya Mbuge wa Jimbo la Kahama James Lembeli ya kusema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) sio mama yake ni kama kitendo cha kuvimbiwa Madaraka aliyokuwa nayo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja alitoa kauli hiyo wakati akiwahutubia wakazi wa Kata Isaka katika ziara yake ya kuzungumzia maendeleo amani na Upendo na katika Wilaya ya Kahama pamoja na kukagua shuguli za maendeleo kama ilani ya chama hicho inavyosema.

Mgeja alisema kuwa wao kama chama cha mapinduzi Mkoa wa Shinyanga wamekuwa wakipokea simu mbalimbali kutoka kwa wadau kulaani kitendo hicho kilichosemwa na Mbunge huyo tena mbele ya vyombo vya habari.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema kuwa Chama cha Mapinduzi ndicho kimemfikisha Mbunge huyo hadi alipo na kimemfanya hadi kupata fursa za kutembelea hadi nchi za nje lakini kwa kauli yakje hiyo aliyoisema inakuwa aileti tija kwa chama hicho ambacho hadi hivi sasa ni Mbunge kupitia CCM.

“Sisi hatuna taabu juu ya mambo mengine yanaymhusu yeye kama kuunga mkono Serikali tatu lakini sisi kama Wananchama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga tunapingana na kauli yake moja tu ya kusema Chama cha Mapinduzi sio mama yake”,Alisema Khamis Mgeja Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

“Leo katika Mkano huu sina nafasi ya kuzungumzia kuhusu kauli ya Mbunge huyu kwani Katibu wa Itikadi na uenezi wa Mkoa alishayasema haya hapo awali na kutuwakilisha uongozi wa Mkoa wa Shinyanga katika kulaanui kitendo cha  Mbunge huyo tena wa CCM”, Aliongeza Khamis Mgeja.

Pamoja na Mambo mengine katika Mkutano huo Mgeja aliwataka watanzania kuungano juu Serikali mbili katika mchakato wa kupata katiba mpya mpya na kuwataka viongozi wa matawi ya CCM kuwaambia wananchi wao juu faida za Serikali mbili badala ya kushabikia Serikali tatu kama walivyo wabunge wa upinzani.

Pia Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga alisema kuwa kitendo cha viongozi kupenda Serikali tatu ni kama mkitendo cha kuwabebesha watanzani mzigo na kuongeza kuwa Serikali tatu ipo pamoja na ukiunganisha Seriali za Mitaa lakini bado watanzania hawajajua hivyo.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply