WAANDISHI WA HABARI NI LULU YA WANYONGE
Na Mohab Dominick
Shinyanga
Imeelezwa kuwa waandishi wa habari hapa nchini ni mkombozi wa
wanyonge hasa pale wanapoandika habari za kijamii na kufichua maouvu
yanayofanywa na baadhi ya viongozi walioko kwenye madaraka kwa kushindwa
kutekeleza miradi ya maendeleo pamoja na kuzitafuna fedha hizo
Hayo yamezungumzwa jana na meneja wa CRDB tawi la shinyanga mjini
Saidi Pamuye wakati akisoma hotuba katika siku ya uhuru wa habari kwa
wanahabari wa mkoani shinyanga katika maadhimisho hayo
Pamuye alisema asilimia kubwa ya jamii hasa wale waishio maeneo ya
vijijini wamekuwa hawapati huduma zao muhimu pamoja na kutendewa matendo maovu
na baadhi ya watu wenye kipato wakiwemo na viongozi wa serikali ambao wamekuwa
wakila fedha za miradi zinazotolewa kuwatekelezea miradi yao
Alisema chombo pekee chenye kuwasemea wanyonge hao kwa serikali na
kuwasaidia kupata haki zao kwa baadhi ya watu wachache wanaohujumu miradi yao
na kuwakandamiza, ni vyombo vya habari ambavyo ndivyo vyenye sauti kubwa ya
kufikisha ujumbe wao kwa walengwa na kuweza kutatulliwa matatizo yao
Akizungumza katika maadhimisho hayo mkuu wa upelelezi mkoani
shinyanga Hussein Kashidye aliwataka wanahabari wa mkoa huo licha ya
kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo bali wafanye kazi kwa ufanisi na
weledi kwa kuzingatia sheria za uandishi na kufichua maovu bila ya kuwa na uoga
Kashidye alisema wanahabari ndio nguzo pekee iliyobaki ya kufichua
maouvu na kuyakemea na kuifanya jamii iweze kuishi kwa amani na upendo hivyo
wanawajibu wa kutafuta habari za uchunguzi huku wakishirikiana na Jeshi la
polisi kwa kupeana taarifa mbalimbali ambazo zitasaidia kuondoa changamoto hizo
kwa wananchi
“wanahabari ndio nguzo pekee iliyobaki ya kufichua maovu
yanayofanyika ndani ya jamii pamoja na serikali kwa kutoa taarifa kwa kupitia
vyombo,na sisi kama Jeshi la polisi tukipata habari hizo tunazifanyia kazi na
pia tunaomba tushirikiane natufanye kazi kwa pamoja kukemea matendo hayo
maovu”alisema Kashidye
Aliongeza ‘licha ya kuandika habari za maovu yanayofanywa na
baadhi ya viongozi wa serikali pia jeshi tunaomba muandike habari za kukemea
mauaji ya vikongwe na Alibino ambayo bado yanaendelea katika mkoa wetu kutokana
na imani za kishirikina,Mila potofu pamoja na kugombania Mirathi”
Naye Afisa vipimo wa mkoa wa Shinyanga Juma Chacha aliwataka
wanahabari wa mkoa huo kuacha kutumiwa na baadhi ya wadau kwa kuandika habari
zenye manufaa yake binafsi kwa kupewa fedha na kuacha kuandika ukweli hali
ambayo itaendelea kuwa didimiza wanyonge na kurudisha maendeleo ya kiuchumi kwa
jamii
“Sasa wanahabari umefika wakati wa kutoa taarifa kwa uhuru
bila ya kujali wadhifa wa mtu wala cheo chake kwa kuandika habari zenye
kufichua maouvu, mfano sisi wakala wa vipimo kipindi cha msimu wa zao la pamba
tumekuwa tukipata wakati mgumu pale tunapofanya kazi yetu ya kukagua vipimo na
kukukata vipimo hivyo vimechezewa na kumuibia mkulima” alisema Chacha
“Na pale tunapowakamata wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya
sheria lakini asilimia kubwa tumekuwa hatusikii habari zao zikitolewa kwenye
vyombo vya habari hali ambayo inatupa wasisi wasi kuwa labda mmepewa kitu
kidogo ilimsitoe habari”mwisho
No comments: