sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » MWALIMU AUWA MWANAFUNZI KAHAMA



Na Mohab Dominick
Kahama
May  6, 2014.

MWALIMU AUWA MWANAFUNZI KAHAMA

MWANAFUNZI  mmoja mkazi wa wa Jijini Mwanza Clinton Majembe ameuwawa kwa kupigwa na mama yake wa kambo Lupinda Kauli Mwalimu wa Shule ya Msingi Malunga mjini Kahama kwa kinachodaiwa kuwa kuwa mtoto huyo aliacha jiko jiko la gesi likiwa linawaka ndani.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Noel Mseven ambapo tukio hilo lilitokea usiku wa kuakia Ijumaa kuu alisema kuwa Marehemu alikuwa ni Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule moja mjini Bukoba.

Mseveni alisema kuwa Marehemu Clinton alikuja kumsalimia mama yake wakati wa likizo ndogo ya pasaka na hivyo kumkosa hali ambayo ilisababisha mama yake huyo wa kambo aliyekuwepo katika nyumba hiyo kupiga kutokana na kudai kuwa alikuwa amewasha jiko la gesi bila ya idhini yake.

Alisema kuwa Mama huyoa ambaye ni mtu wa matukio katika mtaa huo pia inasadikiwa pia aliwahi kmtishia mume wake kumuua na hivyo kusababisha kuukimbia mji wake mpaka kufikia hivi sasa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Ernest Mangala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa kwa sasa hayupo ofisi yupo nje kikazi na kuhaidi kulizunguzia tukio hilo pindi atakaporejea kazini hivi karibuni.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply