sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » ZIMAMOTO KAHAMA WAFANYIA KAZI MAKABURINI



KATIKA hali ya kushangaza iliyojitokeza kwa Jeshi la Zimamoto la Halmashauri ya Mji wa Kahama ni pale ambapo wamekosa ofisi ya kufanyia kazi na kuhamishia katika eneo ambalo linasadikiwa kuwa lilikuwa na makaburi hapo awali.

Jeshi hilo ambalo ni muhimu katika matika matukio ya uzimaji wa moto katika Mji wa Kahama pia wamejikutaa wakikosa ofisi za kufanyia kazi hali ambayo imewafanya kufanyia shughuli zao za kiofisi katika gari lao la kuzimia moto.

Baadhi ya watumishi wa Jeshi hilo wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kuhsu kupatiwa eneo la kufanyia kazi lakini jitihada zao zimekuwa zikigonga mwamba bila ya mafanikio huku wakiendelea kusota katika mazingira magumu ya kufanyia kazi

Akiongea na Habarileo  juzi Mkaguzi wa Jeshi hilo Mkoa wa Shinyanga Rashidi Mwinyimkuu alisema kuwa madai hayo yanayodaiwa na Askari wa jeshi ni ya msingi na kungeza kuwa wamekuwa wakijitahidi kupata eneo la kufanyia kazi lakini mazungumzo bado yanaendeleo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala.

“Unajua ndugu Mwandishi Jeshi la zimamoto katika Halmashauri ya Mji wa Kahama limeanzishwa hivi karibuni baada ya kuzaliwa kwa Halmashari hiyo na kwa sasa tupo katika mkakati mkubwa wa kuhakikisha kuwa tunapata maeneo kwa ajili ya kufanyia kazi Ashari hawa”, Alisema Rashidi Mwinyimkuu.

Pia Mkaguzi huyo aliendelea kusema kuwa kwa sasa Wananchi wa Mji wa Kahama wanahitaji kupata elimu kubwa juu ya matukio yanayohusu moto ikiwa ni sambamba na kutumia vifaa maalumu vya kuzimia moto katika maeneo mbalimbali ya maduka mahotel na sehemu nyingine.

Aliendelea kusema kuwa Wilaya ya Kahama kwa sasa inakuwa kwa haraka zaidi na watu wakiendelea kujenga nyumba nyingi ikiwa ni pamoja na maeneo ya biashara kuwa mengi hali ambayo kwa kuwa na ofisi ya zimamoto katikati ya mji itasadia wa kiasi kikubwa kuwahi matukio.

Hata hivyo Mkaguzi huyo alisema kuwa Changamoto nyingine inayoikabili ofisi yake ya zimamoto ni pamoja na kutokuwa na namba maalumu kwa ajili ya Wananchi kupiga pindi matukio ya moto yanapotokea na kungeza kuwa hali hiyo inatokana na kutokuwa na ofisi maalumu kwa ajili ya kufanyia kazi.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply