sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » WABUNGE WA KATIBA WATAKIWA KUJUA SERIKALI TATU ZIPO NDANI YA SERIKALI MBILI


Na Mohab Dominick
Kahama
May 13, 2015.

WABUNGE WA KATIBA WATAKIWA KUJUA SERIKALI TATU ZIPO NDANI YA SERIKALI MBILI

CHAMA cha Mapinduzi Mkoa Shinyanga kimewataka Wabunge  katika mchakato wa kupata Katiba Mpya Jamhuri ya Muungano kuhakikisha kuwa wanarudisha Madaraka kwa Wananchi kwani suala la Serikali tatu lipo ndani ya Serikali mbili kupitia Serikali za mitaa.

Hayo yalisemwa juzi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja wakati akizungumza na wakazi wa Mji mdogo wa  Isaka katika moja ya kukagua ilani ya Chama hicho kama inatekelezwa.

Mgeja aliwakumbusha Watanzania kuwa Tanzania tayari inazo Serikali tatu ambazo hazina gharama yeyote na kufafanua kuwa Serikali kwanza ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya tatu ni  Serikali za Mitaa.

Alisema kuwa Mfumo ulipo sasa ni wa Serikali tatu ndani ya Mfumo wa Serikali mbili na kuongeza kuwa mfumo huo ni mzuri ambao hauna gharama na mzigo mkubwa  kwa Wananchi wa Tanzania.

Mwenyekiti huyo aliwaomba Wabunge wa Bunge la Katiba pamoja na Watanzania wote kutambua kuwa Serikali ya tatu ipo nayo si Serikali za mitaa ambayo ni Serikali ya Demokrasia na yenye mamlaka kamili kwa Wananchi ambao wamejiamulia wenyewe na kupanga mipango ya maendeleo katika maeneo husika.


“Ninawaomba Watanzania kuwa na Serikali za Mitaa ni jambo la kujivunia kwa kuwa wananchi watakuwa wakijiongoza wenyewe kupitia mabaraza yao ya Madiwani”, Alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa kupitia Mabaraza ya Madiwani kwa sasa wananchi wameweza kufaidika na mambo mengi katika sekta mbalimbali za huduma za kijamii zikiwemo sekta za maji, Afya Elimu, Barabara, Kilimo, uvuvi, Ufugaji na Utamaduni.

Alisema kuwa mambo yote yanayofanyika kwa sasa kupitia Serikali kuu baadhi  ya mambo na majukumu yanaweza kufanywa kupitia Serikali za Mitaa kwa kuwa mfumo ni uleule unatumiwa na kuwataka Wabunge wa Katiba kufikiria kwa makini juu ya mchakato huo unaoendelea ili kuwapa mamlaka kamili wananchi kuliko kuwatwisha mzigo mwingine  wa Serikali tatu wa kuendelea kutawaliwa.

Aliendelea kusema kuwa kuwepo kwa Serikali za mitaa kunatosha kujibu kiu ya watu wanaolilia kuwepo kwa Serikali tatu na kusisitiza kuwa jambo  muhimu kwa wakati huu  amewashauri wabunge wa  Katiba wote bila ya kujali itikadi zao za Vyama na makundi ya uwakilishi kuunga mkono mawazo hayo yenye manufaa kwa Wananchi na Taifa kwa ujmla.

“Kuwepo kwa Serikali za mitaa kunatosha kujibu kiu ya watu wanaolilia kuwepo kwa Serikali tatu na kusisitiza kuwa jambo  muhimu kwa wakati huu  amewashauri wabunge wa  Katiba wote bila ya kujali itikadi zao za Vyama na makundi ya uwakilishi kuunga mkono mawazo hayo yenye manufaa kwa Wananchi na Taifa kwa ujmla”,Alisema Mgeja

MWISHO

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply