sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » MADIWANI WATATU WALA POSHO ZA ZIARA YA MBEYA WAINGIA MITINI WASHINDWA KWENDA ZIARA



UMOJA wa wazee (UWAKA) katika halmashauri ya mji  Kahama umelalamikia Madiwani watatu Bobson Wambula (CHADEMA)  Majengo James Mlekwa (CCM)  Nyahanga na Mussa Mabubu (CCM)  Busoka kwa kudaiwa kuchukua  sh.480,000 posho ya ziara ya Mbeya kujifunza usafi.

Wakizungumza katika kikao chao wazee hao, walisema kitendo walichokifanya Madiwani hao ni kuwadhulumu wananchi kwani fedha waliyochukua jumla ya shilingi 1440,000 na kuacha kwenda ziara ingesaidia kujenga hata  chumba kimoja cha ofisi ya zima moto  kutokana na kikosi hicho kukosa ofisi.

Akizungumzia kero hizo katika kikao hicho kilichofanyika katika Hoteli ya Rockpoint mjini Kahama katibu wa umoja huo Paul Ntelya alisema kuwa hivi karibuni Baraza la Madiwani lilitumia zaidi ya shilingi m.40 kwenda kujifunza usafi katika jiji la Mbeya ambapo niufujaji wa fedha za Serikali.

Aidha Ntelya alisema wao kama wazee wa mji huo wangeshirikishwa wangewashauri kwenda katika Jiji la Mwanza ambako napo wangejifunza usafi pia kutokana na mji wa Mwanza kuwa ni mkubwa na ni msafi hali ambayo wangetumia gharama ndogo.

Alisema kwamba mji wa Kahama unakua kwa kasi ya ajabu lakini Halmashauri ndiyo inachangia kuurudisha nyuma mji huo  kimaendeleo badala wajikite katikla kuboresha vyanzo vya mapato kama Soko kuu linalolalamikiwa kukosa maji,choo pamoja na mifereji ya kupitisha maji.

‘’Halmashauri inatuchukia sana sisi Wazee hasa tunaposema matatizo ya mji  huu sisi hatulalamikii fedha zinazotumika bali tunalalamika kuhusu matumizi mabovu katika halmashauri yetu tunashangaa serikali kutenga kiasi hicho cha fedha milioni 40 kwenda mbali nawengine kuchukua za kuchezea badala ya kwenda  Mwanza ambapo ni karibu wakaokoa milioni kadhaa.

‘’Wanajifunza nini hata wakati ule walikwenda Moshi kujifunza huohuo usafi  hatujaona elimu waliyoitumia kutoka Moshi sasa wamechukua mamilioni ya pesa wamekwenda huko Mbeya huku miundo mbinu ya soko na maeneo mengine ni mibovu wanazidi kuuongezea mji wetu changamoto rukuki’’Alisema Ntelya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Jidula Mabambasi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Zongomera akijibu malalamiko hayo alisema kuwa Suala la kwenda Madiwani wake katika jiji la Mbeya kujifunza Usafi liko kisheria katika Halmashauri zote za miji.

Alisema kutokana na hali hiyo malalamiko yao ameyapokea na atayawasilisha katika Baraza la Madiwani lijalo nakuongeza kuwa siyo wazee tu hata mwananchui wa kawaida anahaki ya kufuatilia mapato na matumizi katika Halmashauri yao.

MWISHO

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply