Baadhi ya vijana ishirini toka halmashauri ya msalala wakiwa katika mafunzo ya wiki moja juu ya ufungaji wa umeme wa mionzi ya juu katika halmashauri hiyo ambapo kampuni ya Rex Energy wakala wa umeme vijijini Rea .
Mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya akisisitiza jambo ya masomo ambayo watapata juu ya ufungaji wa sola za miozi ya jua wakati wa ufunguzi wa semina ya vijana ishirini juu ya ufungaji wa umeme wa mionzi ya jua katika halmashauri ya msalala wilayani kahama .
Mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya akiwahutumbia vijana juu ya semina ya ufungwaji wa umeme wa jua mjini kahama .
Afisa elimu sekondary halmashauri ya msalala ntobi mwenye shati la kitenge akimkaribisha mkuu wa wilaya ya kahama benson mpesya hayupo pichana kwenye semina ya vijana ishirini toka halmashauri ya msalala juu ya ufungaji wa umeme wa jua .
Mkurungezi wa halmashauri ya msalala patrick akitoa shukurani kwa kampuni ya Rex Energy kwa kuleta mafunzo kwa vijana ishirini katika halmashauri yake juu ya ufungaji wa umeme wa jua katika shule za sekondary .
picha ya pamoja
Baadhi ya vijana wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya kahama benson mpesya hayupo picha wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo ya umeme wa jua katika halmashauri ya msalala wilayani kahama .
Mkufunzi wa kampuni ya Rex Energy toka dar es salaam akitoa mafunzo ya ufungaji wa umeme wa jua katika sekondali za halmashauri ya msalala .
SERIKALI Wilayani Kahama imewataka vijana kutumia fursa zinazowazunguka katika maeneo wanayoishi badala ya kukaa vijiweni na kuorodhesha kero zinazozunguka jamii ya eneo usika na kusababisha kuibuka kwa majungu na kudhorotesha kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya aliyasema hayo wakati akifungua semia ya siku ya siku saba iliyoandaliwa na Kampuni ya Rex Energy na kufadhiliwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kwa lengo la kuwafundisha vijana jinsi ya kufunga umeme wa mionzi ya juu maeneo ya Vijijini.
Mpesya alisema kuwa kwa Kapuni hiyo ya Rex Energy kutoa mafunzo hayo kwa Vijana 20 kutoka katika Wilaya Msalala kutasaidia katika vijana wenge kuchangamkia fursa hasa za kufunga umeme wa REA katika maeneo ya Vijijini wanapotokea.
Alisema kuwa kwa sasa Watanzania wengi hususani Vijana wengi wamekuwa na kazi moja tuu ya kuorodhesha matatizo katika jamii inayowazungua huku wakisahau kuchangamkia fursa zinazowazunguka katika maeneo husika
Mpesya alisema kuwa mafunzo hayo kwa Vijana ni kama wamepatiwa nyenzo mahimu ambayo wallitakiwa kuatiwa katika vyuo na hivyo kutumia fedha nyingi hali ambayo Kampuni ya Rex itakuwa imetatua tatizo hilo kwa kiasi fualani.
Kwa upande wake Mhandisi kutoka katika Kampuni ya Rex Energy alisema kuwa Kampuni ya wakala wa Umeme Vijijini itaweka umeme katika shule 16 katika Halmashauri ya Msalala huku mradi huo ukigharimu kiasi cha shilingi milioni 300.
Alisema kuwa Mradi huo utaweza pia kuwapa Mwanga Vijana na kujiona kama nao ni waajiriwa kwa kutumia mafunzo hayo na kutoa msaada mkubwa kwa Wananchi wanahitaji huduma ya umeme vijijini pindi mradi huo utakapoanza.
Pia alisema kuwa vigezo vilivyotumia katika wapata Vijana hao ni pamoja na kuwa na sifa ya Elimu ya kidato cha cha nne pamaoja na wale waliopitia katika elimu ya veta na kuongeza kuwa hii itawasaidia vijana wengi kwani wengi wao wapo majumbani wakiwa hawana kai ya kufanya.
Na Mohab Dominick- Kahama
No comments: