SERIKALI Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwa
kushirikiana na Mgodi wa Barrick Buzwagi imesema kuwa watakuwa mstari wa Mbele
katika kuhakikisha wanawaunganisha Vijana kupitia masula ya Michezo ili
kuhakikisha kuwa Wilaya ya Kahama inakuwa mstari wa mbele katika sekta
nzima ya Burudani na Michezo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya aliyasema
hayo wakati akifunga Bonanzala siku tatu lililoandaiwa na Kampuni ya Mgodi wa
Dhahabu wa African Barrick Gold (ABG) Kupitia Mgodi wa Buzwagi kwa lengo la kuwaunganisha Vijana ikiwa ni
sambamba na kufahamiana.
Lengo lingine kusherekea ufungwaji wa Mashindano ya
Kombe la Dunia yalikuwa yakionyeshwa na Kampuni hiyo kupitia senema katika
uwanja wa Halmashauri hali iliyochangia Wananchi kuangalia mashindano hayo kwa
muda wamwezi mzima bila ya kutoa gharama yeyote.
Alisema kuwa kwa Serikali Wilayani hapa kwa
kushirikiana na wawekezaji hao na kuhakikisha kuwa Wilaya ya Kahama inakuwa na
kusonga mbele katika masuala ya michezo hususani Mpira wa Miguu ambao umepoteza
mwelekeo tangu iliposhuka daraja timu ya Kahama united.
Alisema kuwa Serikali inatambua uwepo wa wawekezaji
katika Wilaya ya Kahama na kuongeza kuwa wataendelea kushirikiana katika
masuala mbalimbali ikiwa ni sambamba na michezo ili kuinua vipaji kwa wakazi wa
mji wa Kahama.
“Msi waogope wawekezaji kwani wao sio Wanyama ni
binadamu kama sisi tushirikiane ili tukuze michezo katika Mji wetu ambao kwa
sasa unakuwa kwa kasi na tunatakiwa kuwa ni timu katika ligi kuu huko
tuendako”, Alisema Benson Mpesya Mkuu wa Wilaya ya Kahama.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa
Buzwagi (ABG) Amos John alisema kuwa Kampuni yake itaendelea kutoa ushirikiano
kwa vijana wa Mji wa Kahama na kuongeza kuwa wapo tayari katika kuhakikisha
wananchi wa Kahama wanajenga mahusiano mazuri na Mgodi
Na Mohab Dominick-Kahama
No comments: