sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » MICHIGANI MALUNGA YAPIGWA JEKI VIATU NA JEZINa  Mohab Dominick
Kahama
Agust 11, 2014.


MTANZANIA Mkazi wa Kahama anayefanya kazi katika Mgodi wa Dhahabu Ruvana Nchini Zambia Majaliwa Benard juzi alitoa msaada wa jozi 11 za viatu vya mpira wa miguu kwa Timu ya Michigani ya Kata ya Malunga Mjini hapa kwa lengo la kuinua vipaji katika kata hiyo.

Akikabidhi Msaada huo kwa Nahodha wa Timu hiyo ya Michigan Huseini Idd Majaliwa alisema kuwa ameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa vijana hao waliokuwa wakifanya mazoezi katika shule ya Msingi Malunga huku wengi wao wakiwa hawana viatu.

Alisema kuwa yeye katika Maisha yake anapenda sana michezo na kuongeza kuwa hata kama yupo mbali na Kahama hata sita huonyesha ushirikiano katika suala zima la michezo katika timu hiyo ili kuinua vipaji ambayo kwa huku mbali sio rahisi kuvigundua.

Aidha Majaliwa aliendelea kusema kuwa vipaji vipo mijini tuu kama watu na wanamichezo wengi walivyozoea bali hata katika aneo ya Vijijini pia kuna vijana wenye vipaji huku akiwataka viongozi wa michezo wa ngazi za juu kutemblea katika maeneo hayo na kujionea.

Mfadhili huyo alisema kuwa jozi hizo 11 za viatu alivyotoa kwa timu hiyo vina jumla ya shilingi 385,000 hali ambayo itasaidia kwa vijana hao katika kuendeleza vipaji  vyao na hivyo kutimiza ndoto zao walizojiwekea siku za baadaye katika masuala mazima ya mchezo wa Mpira wa miguu.

Wakati huo huo msaria mwema Baraka Alli nae alito seti moja ya jezi kwa timu hiyo kama kumuunga mkono Majaliwa katika jitihada za kuhakikisha kuwa timu hiyo ya Michigan FC ya Malunga inafanya vizuri katika michezo yake.

Nae Nahodha wa Timu hiyo Husen Alli akipokea msada huo alisema kuwa wamefurahishwa na watu hao wenye mapenzi mema kuwa na moyo wa kusaidia na kungeza kuwa mbali na kupta misaada hiyo bado wanakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa mipira na kuwataka wafanyabiashara wengine kujitokeza katika kutatua tatizo hilo.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply