mama huyu mkazi wa kata ya ushetu wilayani kahama akiwa muda mfupi baada ya kujifungua mtoto wa kike hospitali ya wilaya ya kahama ilalamikiwa kwa kutoa huduma hafifu kwa kinamama wajawazito kwa huduma hiyo lazima kutoa kitu kindogo cha shilingi elf tano mpaka kumi .
Na Mohab
Dominick
Kahama
Agosti 11,2014
WAGONJWA
wanaolazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga hususuani
katika wadi ya watoto wamekuwa wakijikuta wakipoteza maisha mara kwa mara kwa
kinachodaiwa kuwa ni huduma mbovu zinazotolewa na Wahudumu wa Hospitali hiyoikiwa
ni sambamba na kukithiri kwa Rushwa.
Baadhi ya Wazazi wamekuwa wakilalamika kila
siku kuhusu uongozi wa Hospitali hiyo bila ya tatizo hilo kufanyiwa kazi kwa
kipindi muafaka hususani katika wadi ya watoto ambayo ndio yenye wagonjwa wengi
hadi kufikia kulala kitanda kimoja wagonjwa wanne.
Wakizungumza na
Mwandishi wa Habari hizi aliyetembelea
Hospitali hapo juzi, wagonjwa hao walisema kuwa kauli chafu,rushwa kwa baadhi
ya manesi ni miongoni mwa sababu zinazopelekea kutokea kwa vifo vya
watoto ambavyo visivyokuwa vya lazima hali ambayo inapaswa kukemewa mara moja
ili kuondoa tatizo hilo.
Akizungumzia hali
hiyo kwa masikitiko makubwa mmoja wa wagonjwa aliyelazwa na mtoto wake katika wodi ya watoto Joyce
Richard alisema kuwa pasipo kutoa chochote yaani fedha kwa wauguzi wa wadi hiyo
huwezi kupata huduma kwa wakati hali
ambayo ilipelekea mtoto wake wa kwanza kufaliki dunia akiwa
hospitalini humo wakati akipatiwa matibabu.
Aidha alisema
kuwa kuwa kuna baadhi ya watoto katika wadi hiyo wempoteza maisha maisha huku
wakiwa na uwezo wa kupata huduma bora hali ambayo alisema imekuwa ikiwakatisha
tama hata katika kuwaleta watoto wao katika Wodi hiyo kutokana na huduma mbaya
zilizopo katika wadi hiyo tena ya watoto.
“Mimi nililazwa
na Mtoto wangu katika kitanda kimoja tukiwa wanne na mimeshuhudia zaidi ya
watoto nne katika wodi hiyo wakipoteza maisha kwa uzembe wa wahudumu wa wodi
hiyo hali ambayo inasikitisha kwa kweli, na kwa nini watoto wetu wapoteze
maisha kizembe namna hiyo?”,Alihoji Joyce Richard
Alisema kuwa
kiwango wanachotozwa na baadhi ya manesi hospitalini humo ni kuanzia shilingi
5,000 hadi 10,000 kwa wale wenye uwezo na kuongeza kuwa mtu anayetoa kiwango kikubwa cha pesa ndio
anayeboreshewa huduma za matibabu na manesi hao ikiwa ni pamoja na kutembelea
mgonjwa husika mara kwa mara kujua hali yake.
Nae Magreth Peter
alisema kuwa baadhi ya manesi wamekuwa na kauli za matusi , mara tu
wanapohitajika katika kuangalia hali za wagonjwa hasa pale zinapokuwa
zimebadilika na kuongeza kwamba inakuwa vigumu kwa mgonjwa kupewa kitanda
wakati wa mapokezi hali ambyo inapelekea watoto hao kulala kitanda kimoja hadi
kufikia wanne.
Aidha kwa upande
wake Mganga Mfawidhi wa hospital hiyo Joseph Fwoma alipoulizwa kuhusu
malalamiko ya wagonjwa hao alikanusha nakudai kuwa wagonjwa wamekuwa
hawafikishi malalamiko yao katika ofisi yake na kuongeza kuwa wamekuwa
wakilalamika tuu nje ya ofisi.
Mwisho.
No comments: