Na Mohab Dominick
Sept 10,2014
Geita-Bukombe.
Afisa Elimu msingi Wilaya ya
Bukombe Shadrack Kabanga amesema kuwa wmepokea taarifa toka kwa wasamalia wema
ambao walimtumia ujumbe kwa sms kuhusu mzazi wa mwanafunzi Shija Athanas Lusesa
ambaye ni athanas Lusesa mkazi wa kijiji cha Ihulike kata ya ushirombo kuwa
amemzuia binti yake huyo asiende kufanya mtihani na kweli hakufanya mitihani yote ya septemba 10 .
Baada ya kupokea taarifa hizo jioni
majira ya saa kumi alichukuwa hatua ya kwenda shuleni Ihulike kujiridhisha na
kukuta kweli mwanafunzi huyo hakuwepo shuleni kushiriki na wenzake kufanya
mtihani ingawa alikuwa amejiandaa na dawati la kufanyia mtihani.
Afisa elimu amesema baada ya kujiridhisha amechukua hatua
ya kwenda polisi kuchukua Askali na
kumkamata mzazi huyo na hadi sasa yuko mikononi mwa polisi baada ya mitihani
kumalizika watamfikisha mahakamani kujibu mashitaka.
Aidha Kabanga amesema kuwa
mwanfunzi Shija Athanas atafanya mitihani iliyosalia akishirikiana na wenzake
kwa kuwa yeye yuko tayari kufanya mtihani.
Afisa elimu Kabanga ametoa wito kwa
wazazi wote wenye tabia kama hiyo waache mara moja kwani serikali imejipanga
kukabiliana na wazazi ama watu wanaotaka kuwazuia watoto wa kike kupata elimu
ya msingi na sekondari.
Amesema Athans Lusesa atakuwa wa
mfano kwa wazazi wengine wenye tabia
kama hizi hasa sehemu za wafugaji kwani limekuwa ni jambo la kawaida kwa wazazi
kuwaachisha masomo watoto wa kike na kwenda kuwaoza ili kujipatia Mali.
Aidha mkuu wa wilaya ya Bukombe
amani mwenegoha amelaani vikali kitendo hicho kilichofanya namzazi huyo kwa
lengo la kujipatia mali nakusema”sisi kama serikali ya wilaya naserikali kuu
kwa ujumla wake inakemea vikali vitendo vya wazazi kama hawa wanaozuia jitihada
za serikali kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu’
Akifafanua zaidi mkuu wa wilaya
amesema kuwa serikali haitavumilia vitendo kama hivi hasa katika maeneo ya
wafugaji ,wachimba madini watu
wanaohamahama ovyo ili kuharibu utaratibu wa elimu hasa maeneo ya ufugaji.
Amesema kuwa kwa kuwa mwanafunzi
Shija Athanas ameshindwa kufanya mitihani ya awali basi serikali itahakikisha
atafanya mitihani yake yote baada ya kutengewa siku yake pekee na huku yeye
babayake mzazi aliyesababisha hayo atashikiliwa na hatimaye kufikishwa
mahakamani kujibu tuhuma za kumzuia mwanafunzi kufanya mtihani wake wa kuhitimu Elimu ya
msingi.
Jumla ya wanafunzi 3731 wilayni
Bukombe mkoani Geita wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi
mwaka huu ambayo iliayoanza tarehe 10 hadi 11 mwezi septemba.
MWISHO
No comments: