Moja ya matangazo ya halmashauri ya mji wa kahama kama livyokutwa na blog hii
chumba hichi ni mjasilimali ambacho amewekea pingamizi ujenzi wake.
hivi ndivyo vibanda ambavyo vinalalamikiwa na wafanya biashara wadogo wa hili soko la samanga .
hivi ndiyo vibandani vya mbele vya soko la samanga ambavyo vimemilikiwa na viongozi wa halmashauri ya mji na madiwani .
majengo ya soko la samanga kwa mbele .ambayo kuna baadhi ya viongozi na madiwa wa halmashauri kujimilikisha kwa mbele .
tangazo kama hili ndiyo yalivyotukamika kwa wateja walichelewa kufanya matengenezo .
huku ni nyuma kwenye hili soko la samaga ambalo bado ujenzi wake hukiwa bado kama hunavyonekaka hapo .
jengo la soko la zamani ambalo limechukuwa zaidi ya miaka mitatu ambapo kumesababisha mvutano mkubwa kati ya wafanyabiasha na madiwani na viongozi wa halmashauri ya mji .
haya majengo ya soko la samanga ambayo ujenzi wake hunasuasua mpaka sasa kuhusu ujenzi huu na kusababisha msunguano mkubwa .
Na Mohab Dominick
Sept 11,2014
Kahama
WANANCHI Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wamewalalamikia
viongozi wa Halmashauri ya mji wa Kahama pamoja na baadhi ya Madiwani
wake kujilimbikizia vibandavya soko la Namanga hali inayowafanya kubaki kuwa
wapangaji.
Akiongea juzi na wandishi wa Habari ofisini kwake,katibu mwenezi
wa chama cha Tanzania Democratic part Aliance(TADEA) wilayani Kahama,Vicent
Manyambo aliwaeleza wandishi wa Habari kuwa wananchi walifika ofisini kwake
kulalamika kwa kuwatuhumu viongozi hao pamoja na madiwani wake.
Aidha manyambo alisema kuwa yeye pia ni shuhuda wa hali hiyo na
kumtaja mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Felix kimaryo kuwa anamiliki vibanda 6
na wengine ni madiwani wa kata ya kahama mjini, Abass omary kumiliki vibanda 6
Bobson Wambula vibanda 6 kwa jina la mke wake.
Pia alisema mwingine ni Diwani wa kata ya Nyihogo,Amos Sipemba
anamiliki vibanda viwili kutokana na kutokuwa mjanja na mwingine ni
aliyekuwa afisa biashara wa mji huo,Boniphace Bulali kuwa naye anavibanda
vyake katika soko hilo na kwamba wajilimbikizia vibanda hivyo na kusababisha
wananchi kukosa hali inayowalazimu wawe wapangaji wao.
Hata hivyo manyambo alisema kuwa Halmashauri ya mji huo imekuwa
ikiwahamisha kwa nguvu wafanyabiashara hao kutoka katika maeneo yao ya biashara
kwakile walichodai kuwa hayo si masoko rasmi ili kuwapeleka katika soko hilo la
Namanga ili wawe wapangaji wao.
Alisema mkurugenzi pamoja na madiwani hao wamejilimbikizia vibanda
hivyo ambapo wafanyabiashara ambao ndio walengwa hawana vinda katika soko hilo
licha ya kumiliki vibanda huko walikotolewa na kwamba wameamua kufikisha
malalamiko yao kwa chama hicho ili kiwasaidie.
Akijibu tuhuma hizo Afisa Biashara wa mji huo,Sarah Mlagwa alikanusha
madai hayo ya katibu wa TADEA kuwa si ya kweli nakusema kuwa Halmashauri
kutokana na tangazo lake la ujenzi wa vibanda wananchi wote waliochukua fomu
hizo ndiyo wanaotambuliwa kuwa ni wamiliki wa vibanda.
Mlagwa alisema hata hivyo baadhi ya watu walijaza fomu hizo
walishindwa kukamilisha majengo yao kwa muda uliopangwa na Halmashauri yake
ambapo wengi wao waliamua kuviuza kwa watu wenyeuwezo wa kukamilisha kwa muda
ulopangwa nakuongeza kuwa hali hiyo ya wananchi kuuza vibanda vyao ilimchanganya
katika kuandaa mikataba yao.
Kwa upande wao Madiwani wanotuhumiwa wakiongea na gazeti hili kwa
nyakati tofauti wamekanusha madai hayo ambapo wamesema kwamba wao hawana
vibanda katika Soko hilo licha ya kuwa baadhi yao wanaishi jirani na soko hilo
nakudai kuwa hizo ni chuki binafsi za vyama na kuwachafua kisiasa hasa kwa
kuona siku za uchaguzi zimezidi kusogea.
Mwisho.
No comments: