Mwenyekiti
wa kanda ya Ziwa Victoria, Mashariki jimbo la maswa mashariki Silyvester Kasulumbayi, alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya nyihongo mjini kahama .
Mbunge wa jimbo la maswa mashariki Silyvester kasulumbayi akionyesha katiba iliyopendekezwa na bunge la katiba kuwa siyo sahihi katika viwanja vya nyihongo mjini kahama .
Viongozi na wanachama wakisikiliza hotuba ya mbunge wa maswa mashariki katika viwanja vya nyihongo mjini kahama .
Mbunge wa maswa mashariki akisisitiza jambo juu ya katiba iliyopendekezwa na bunge la maalum la katiba .
Akijibu
swali juu ya alama ya bendera ya Chadema kuwa na rangi nyekundu na vidole
viwili,Mwenyekiti huyo aliwatoa hofu wananchi juu ya bendera yenye rangi
nyekundu kuwa inaashiria hatari na umwagaji damu,na ile alama ya vidole viwili
kuwa ni chama cha wezi na kudai kudai kuwa, rangi nyekundu inashiria upendo.
CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo(CHADEMA),kanda ya Ziwa Victoria Mashariki, kimewataka walimu katika
mikoa ya Shinyanga,Simiyu na Mara wasikubali kuchangia shilingi 10,000 kutoka
katika mishahara yao kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya sekondari za kata.
Pia Chama hicho kimewataka wafanyabiashara nao wasikubali
kulazimishwa kuchangia michango hiyo kwa vile hilo ni jukumu la serikali
kuhakikisha inatekeleza ahadi zake katika ujenzi wa maabara kama Chama Cha
Mapinduzi kilivyo ahadi katika ilani yake ya uchaguzi.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama hicho kanda ya Ziwa
Victoria Mashariki,Silyvester Kasulumbayi, jana alipokuwa akiwahutumbia
wananchi wa mji wa Kahama katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja
vya Nyihogo mjini humo.
Kasulumbayi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Maswa Mashariki
(Chadema),alisema,ujenzi wa maabara hayo ni jukumu la serikali iliyoko
madarakani na michango kutoka kwa mwananchi yeyote ni wa hiyari,kama ulivyo
mchango wa harusi.
Alisema walimu na wafanyabiashara wasikubali kulazimishwa kutoa
fedha hiyo kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa maabara,kwa lengo la kutekeleza
agizo la wakuu wa wilaya baada ya kuamriwa na Rais Jakaya Kikwete,kukamilisha
ujenzi huo ndani ya mwezi wa oktoba.
Akijibu swali la mmoja wa wananchi katika mkutano huo,
Kasulumbayi alisema kuwa,inashangaza kuona serikali ya CCM imetumia mabilioni
ya fedha kwa ajili ya bunge maalum la Katiba,kwa kuwalipa wajumbe wa bunge hilo,na
kutunga katiba isiyo na tija kwa watanzania,na kuwa ingekuwa busara serikali
kutumia mabilioni hayo kujenga maabara na siyo kulazimisha michanago kutoka kwa
wananchi.
“ndugu zangu walimu,msikubali kuchangia shilingi 10,000,na
ninyi wafanyabiashara,hilo ni jukumu la serikali,serikali isingetumia mabilioni
ya fedha kwa bunge maalum la katiba na kutunga katiba isiyo na tija, ingetumia
fedha hizo kujenga maabara’alisema Kasulumbayi.
Mwenyekiti huyo pia aliwataka wafanyabiashara wasikubali
kuchangia michango hiyo kwa lazima,kama inavyoamriwa kwani michango hiyo ni ya
hiyari kama michango mingine.
Akizungumzia Katiba mpya Mwenyekiti huyo aliwataka wananchi
kutoiunga mkono,na kuwataka walimu kuunga kampeni ya Chadema kuipinga katiba
hiyo na kuwataka walimu watumie njia ya simu kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu za
kiganjani (SMS),kupinga Katiba hiyo.
Kuhusu uchaguzi ujao Mwenyekiti huyo alisema kuwa,wananchi
hawanabudi kuunga mkono UKAWA ambayo wameamua kusimamisha mgombea anayekubalika
katika kila eneo husika na kuwa umoja huo utadumu katika changuzi zote kuanzia
zile za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao na kuwahimiza wananchi
kujitokeza kwa wingi kujiandisha katika daftari la wapiga kura.
Akijibu swali juu ya alama ya bendera ya Chadema kuwa na
rangi nyekundu na vidole viwili,Mwenyekiti huyo aliwatoa hofu wananchi juu ya
bendera yenye rangi nyekundu kuwa inaashiria hatari na umwagaji damu,na ile alama
ya vidole viwili kuwa ni chama cha wezi na kudai kudai kuwa, rangi nyekundu
inashiria upendo kwani hata siku ya wapendao duniani ambao watu huvaa nguo
nyekundu, na vidole viwili vinavyoelekezwa juu siyo wizi,bali ni alama ya
mshikamano na ushindi.
Mwisho.
No comments: