Hii ni moja ya picha mbalimbali za wajawazito kama inavyonekani siyo ya mwalimu muhusika kwa tukio hilo.
WAKATI ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume
huwarubuni wanafunzi wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za
kielimu kutokana na kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako
mwanafunzi wa Kidato cha Pili anadaiwa kumzalisha mwalimu wake.
Mwanafunzi
huyo aliyemzalisha mwalimu wake ana umri wa miaka 17, wakati mwalimu huyo
anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya Umma ya Nkasi, iliyopo mwambao mwa
Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, Rukwa, ana umri wa miaka 25.
Tukio
hilo linalotajwa kuwa la kwanza kutokea wilayani hapa, limekuwa gumzo kubwa kwa
wakazi wa Nkasi na wilaya jirani.
Hata
hivyo, kwa wanafunzi, wamekuwa wakimpongeza mwenzao kwa kujaliwa kupata mtoto
katika umri wake huo mdogo, huku mzazi mwenzake akiwa na uhakika wa maisha
kutokana na kuwa ni mtumishi serikalini.
Imeelezwa
kuwa licha ya tukio hilo, mwalimu huyo aliyezaa na mwanafunzi wake bado
anaendelea na masomo shuleni hapo, huku `mzazi’ huyo wa kiume akifundishwa na
mzazi mwenzake.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mjini Namanyere hivi karibuni, Mkuu wa Shule ya
Sekondari Nkasi mjini Namanyere ambayo ni ya mchanganyiko ya umma, Amiamie
Nanga alisema mwalimu huyo alianza kazi shuleni hapo ikiwa ni mara yake ya
kwanza kufundisha baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu chuoni.
“Yameshatokea,
lakini haileti picha nzuri sana, lakini mimi nina uzoefu mkubwa na wakazi wa
mwambao wa Ziwa Tanganyika, kwao si ajabu kuwa na uhusiano na watu waliowazidi
umri, iwe kwa mtoto wa kike au wa kiume, wote ni sawa tu…
“Lakini
katika kisa hiki, inaonesha walimu sasa wanapoteza haiba ya ualimu. Hii kazi
ina miiko na maadili yake …kwa mwalimu huyu hii ni ajira yake ya kwanza,
nikimaanisha ni kituo chake cha kwanza cha kazi tangu ahitimu masomo
yake…” alisema.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema hakuna
kosa kwa mwalimu huyo wa kike kwa kuwa tayari ni mtu mzima.
“Isitoshe
katika kisa hiki ni nadra kumpata mlalamikaji … Mwalimu mwenyewe huyu wa kike
hawezi kuwa tayari kujidhalilisha kuwa amebakwa, yalikuwa maamuzi yake.”
Aliongeza
kuwa, kwa mwalimu huyo kupata ujauzito wa mwanafunzi wake hakuwezi kuathiri
ajira yake, tofauti na mwalimu wa kiume akimpatia ujauzito mwanafunzi wake wa
kike ambaye huathirika kwa kukatisha masomo.
Jitihada
za kumpata mwalimu huyo wa kike na mwanafunzi huyo zimegonga mwamba baada ya
watu wao wa karibu kumweleza mwandishi kuwa hawako tayari
kuuzungumzia mkasa huo.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule hiyo waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi kwa masharti
ya kutoandikwa majina yao kwa hofu ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu
shuleni hapo, pamoja na kukiri kutambua uhusiano baina ya mwanafunzi mwenzao na
mwalimu wao, lakini walisema hivi sasa mwalimu huyo amesitisha uhusiano na
mwenzao na kuanzisha uhusiano mpya na mwalimu mwenzao.
Walisema
pamoja na mambo mengine ni kama mwanafunzi mwenzao ameathirika kisaikolojia
baada ya ‘kupinduliwa’ na mwalimu wake wa kiume ambaye kwa sasa ndiye baba
mlezi wa mtoto.
“Huyu
mwalimu wa kike sisi sasa tunamwita shemeji yetu alikuwa na uhusiano wa
kimapenzi na mwenzetu… penzi lao lilikolea hadi sasa ameweza kumzalia mtoto
huyo…, lakini kwa sasa inavyoelezwa ni kwamba penzi limehamia kwa mwalimu
mwenzake,“ alisema
mmoja wao.
Baadhi
ya watu wa karibu na mwanafunzi huyo wanakiri kuwa mwanafunzi huyo hana uwezo
wa kifedha kumudu kumpatia malezi stahiki mtoto wake huyo, hivyo hata mzazi
mwenzake alipoanza uhusiano na mwalimu mwenzake hakuwa na jinsi, bali
kukubaliana na matokeo.
“Usiniandike
jina, sisi tunashauri mwalimu huyo wa kike na mpenzi wake huyo wa kiume ambaye
ni mwalimu mwenzake wahamishiwe shule nyingine kwa sababu kama kioo katika
jamii wameteleza kwa kiasi kikubwa na watashindwa kuwajenga na kuwalea
wanafunzi wao kimaadili.
“Isitoshe
tunajiuliza sheria hapa inasemaje maana kama angekuwa ni mwalimu wa kiume
amempatia mwanafunzi wake wa kike ujauzito angeshitakiwa na kufikishwa
mahakamani na pengine kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka 30 jela, sasa kwa
hili sheria inasemaje?”Alihoji.
Baadhi
ya wazazi mkoani hapo waliohojiwa na mwandishi kwa nyakati tofauti wameelezea
kushangazwa na tukio hilo, na hasa kwa jinsi mwalimu alivyoshindwa kujizuia
`kujiachia’ kimapenzi kwa mwanafunzi wake.
Mwisho
No comments: