SERIKALI
ZA VIJIJI ZIKAGUE PAMBA KABLA YA KUUZWA
WADAU
pamoja na Wanunuzi wa zao la Pamba Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wameziomba
Serikali za Vijiji katika msimu ujao wa ununuzi wa zao hilo kukagua Pamba
kabla ya kufikishwa sokoni ili kuepusha kuwepo kwa pamba chafu na zinazowekewa
maji na Michanga.
Meneja Kampuni ya ununuzi wa zao la Pamba ya
KCCL Wilayani Kahama Bahati Mayala alisema kuwa kwa kushirikishwa viongozi wa
Serikali za vijiji katika kukagua Pamba kabla ya kufikishwa sokoni kunaweza
kusaidia pamba ya tanzana kurudi katika soko la kimataifa kama ilivyokuwa
zamani.
Malaya
alisema kuwa kwa sasa Changamoto kubwa inayowakabili wanunuzi wa zao hilo ni
pamoja wakulima wengi kuweka maji pamoja na mchanga ili kuongeza uzito wakati
Pamba inapokuwa sokoni hali inafanya zao hilo kushuka ubora wake katika soko la
Dunia.
Alisema
kuwa kwa kushirikiana na uongozi wa serikali za Vijiji katika kukagua Pamba
kama ilivyokuwa miaka ya nyuma inaweza kuwa suluhisho sahihi na kupunguza
uchafy katika zao la Pamba ambalo kwa sasa linaonekana kupteza mwelekeo hasa
katika kanda ya ziwa ambapondipo lilikuwa likilimwa kiasi kikubwa.
Mayala
alizitaja baadhi ya Wilaya ambazo ndizo zimekuwa kinara wa kuchafua Pamba kuwa
ni pamoja na Kishapu, Meatu, Igunga pamoja na Maswa na kuongeza kuwa Wilaya ya
nzega ndio pekee ambayo imekuwa kitoa Pamba safi tofauti na nyingine.
Pia
Meneja huyo aliitaka Serikali kutunga sheria ya kutaka pindi Mkulima
anapobainika kuchafua Pamba kwa makusudi achukuliwe hatua kali za kisheria kwa
kuwatumia wataalu wake yaani maafisa ugani waliopo katika maeneo husika hali
ambayo itakuwa ni chachu kwa wakulima kuuza Pamba iliyo safi.
Akizungumzia
kuhusu kilimo cha Mkataba Meneja huyo wa Kampuni ya KCCL alisema kuwa kilimo
hicho kimeku kigumu kutokana na baadhi ya Wakulima kukwepa kulipa madeni hali
ambayo inakuwa ikitia hasara Makampuni ya ununuzi wa zao huilo la Pamba.
Aidha
alisema kuwa katika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wanadai jumla ya madeni ya
shilingi milioni 80 zinzotokana na mikopo ya Pembejeo, Mbegu pamoja na dawa na
hivyo kuisababishia Kampuni hiyo hasara kubwa huku Kampuni hiyo ikisambaza
mbegu tani 15,000 katika msimu uliopita.
mwisho
No comments: