mabango ya walimu yanayohusu mapujo ya mishahara yao
Bukoba.
Maandamano ya
walimu kuingia katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuadhimisha Siku ya Walimu
Duniani, jana yalipata mtafaruku baada ya polisi kuyaingilia na kuchana bango
mojawapo lililohoji posho za wajumbe wa Bunge la Katiba.
Bango hilo la
kitambaa cheupe lilikuwa na maandishi yanayohoji posho ya Sh300,000 waliyokuwa
wanapata wajumbe wa Bunge la Katiba, yakilinganishwa na kazi kubwa wanayofanya
walimu.
Ujumbe wenyewe
ulisomeka hivi: “Haki iko wapi usawa uko wapi, posho ya mjumbe wa Bunge la
Katiba kwa siku shilingi laki tatu, mshahara wa mwalimu shilingi 370 kwa mwezi.
No big results without big salary (Hakuna matokeo makubwa bila mshahara
mkubwa)”.
Ujumbe huo ulikuwa
ukifanya rejea ya viwango vya malipo ya Sh300,000 kwa siku ambazo walikuwa
wakilipwa wajumbe wa Bunge Maalumu zikiwa ni Sh230,000 kama posho ya kujikimu
na Sh70,000 ambazo ni posho ya vikao.
Hata hivyo bango
hilo lilichanwa hatua chache kabla ya walimu hao hawajaingia uwanjani humo,
ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mwenyekiti wa
Chama cha Walimu Tanzania (CWT), mkoani Kagera Dauda Bilikesi, alisema amesikia
habari za bango hilo kuharibiwa lakini akasema asingezungumza kwa kina kuhusu
suala hilo kwa kuwa hayo yamepita.
Waibuka na
shairi.
Muda mfupi baada
ya polisi kuharibu bango hilo lisionekane uwanjani, walimu hao walipiga chenga
kiana wakaibuka na ujumbe ule ule kwa njia ya shairi.
Kupitia shairi
hilo liliposomwa mbele ya Pinda, walimu walihoji ukubwa wa posho za wajumbe wa
Bunge la Katiba zikilinganishwa na mshahara wanaopata, hali iliyosababisha
umati wa walimu uliokuwa uwanjani hapo kulipuka kwa sauti kubwa za shangwe.
Shairi hilo
lililosomwa na Mwalimu Betwel Magoso kutoka Wilaya ya Biharamulo, lilisababisha
kuvurugika kwa muda kwa utaratibu uliopangwa kwa mujibu wa ratiba, pale
alipohoji wajumbe wa Bunge la Katiba kupata Sh1 milioni kwa siku tatu ambazo ni
mkopo wa mwalimu kwa miaka mitatu.
Mwalimu Magoso
alimgusa Pinda ambaye kabla ya kuanza hotuba yake alianza kwa kusema kuwa
mwalimu huyo alitumia ujanja kufikisha ujumbe wake na kuwa baadhi ya maneno
katika shairi lake yalikuwa ni mazito.
Mwisho.
No comments: