Mwanamke
mwenye umri wa miaka 60 aliyekatwa sehemu zake za siri (nyeti)Akiwa wodi katika hospital ya mkoa wa Tabora .
MME AKATA NYETI ZA MKEWE NA KUPELEKA KWA
SANGOMA.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aliyekatwa
sehemu zake za siri (nyeti) na mumewe anayefahamika kwa jina moja la Mashaka.
Wito umetolewa kwa wananchi kuwa mstari wa
mbele kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahalifu pindi vinapotokea
vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio
hilo baya, mama huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora,
Kitete ambapo anadaiwa kukutwa na kisanga hicho hivi karibuni.
Mwanamke huyo anadai kujeruhiwa na
mumewe usiku wakati wakiwa wamelala nyumbani kwao Mtaa wa Kazaroho Kata ya
Mbugani, Manispaa ya Tabora.
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu akiwa
wodini kwenye hospitali hiyo akiwa na maumivu makali, mama huyo alikuwa na haya
ya kusema:
“Siku ya tukio, nakumbuka mume wangu
alikwenda kutembea, aliporejea nyumbani alifuatana na mtu mmoja ambaye ni
mganga wa kienyeji.
“Walipofika nyumbani aliniambia yupo
na mganga wa kienyeji ambaye alikuwa akitafuta viungo vya sehemu za siri za
mwanamke akiwa na fedha milioni tano. Mimi
nilikataa baada ya kunishawishi lakini usiku nilipokuwa nimelala, mume wangu
alinikata huku akiniamuru nisipige kelele kwa kuwa alikuwa ameshapatana bei na
kwamba ulikuwa ni utajiri mkubwa.”
Alisema baada ya tukio hilo
alijikuta amelazwa hospitalini hapo hivyo hajui kama mumewe huyo alishakamatwa
au la.
Kwa mujibu wa majirani zao, Mtaa wa Kazaroho,
lilikuwa ni tukio la kutisha kwani wasamaria wema ndiyo waliomkimbiza mama huyo
hospitalini ili kuokoa uhai wake.
Majirani hao walimtaka Waziri wa
Maendeleo ya Wanawake Jinsia na Watoto, Sophia Simba kufanya kazi ya ziada ili
sheria ichukue mkondo wake ili kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake
na watoto vinavyoshamiri kwa kasi nchini.
Mmoja wa madaktari hospitalini hapo ambaye
hakutaka kutajwa jina kwa kuwa si msemaji, mama huyo alifikishwa hospitalini
hapo akiwa katika hali mbaya lakini baadaye alipata nafuu hivyo anaendelea
vizuri na matibabu. Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP
Suzane Kaganda aliyehamishiwa mkoani hapa hivi karibuni hazikuzaa matunda hivyo
zinaendelea
No comments: