Baadhi ya kinadada wanafanya biashara za ngono.
Mmoja wa dada poa akiwa katika ofisi yake kusubiri wateja wake.
Tupo kazini ndiyo maneno ya kinadada poa wakiwa nje ya uwanja wa maduka mengi mjini shinyanga .
Best hali ni mbaya hayo ndiyo maneno yakinadada hawa wakitafakali juu ya maisha kuwa ngumu baada ya mkuu wa mkoa wa shinyanga kupinga marufuku biashara hiyo ya ngono katika mkoa wa shinyanga na wilaya zake .
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga;Ally Nassoro Rufunga,mkono
wake wa kushoto anayeonekana ni Mkuu wa wilaya ya Kahama;Benson Mpesya.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga;Ally
Nassoro Rufunga,amepiga marufuku biashara ya ngono inayoshika kasi katika
Halmashauri za Manispaa ya Shinyanga na ya Mji wa Kahama kwa kuziagiza mamlaka
zinazohusika kufuata mkondo wa sheria dhidi ya matendo hayo.
Rufunga alitoa agizo hilo katika
kikao Baina yake na Asasi zisizo za kiraia zinazojihusisha na mapambano dhidi
ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi wilayani Kahama,
ambapo alipatiwa utekelezaji wa
shughuli na changamoto zinazozikabili Asasi hizo katika mapambano dhidi ya
Ukimwi. Moja wa wanaojiuza Alisema vita
hivyo vya mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya Ukimwi katika Mkoa wa
Shinyanga inaathiriwa na kuwepo kwa jamii iliyojitosa kuanzisha madanguro na
kufanya biashara ya ngono.
Aidha aliziomba Asasi zinazojihusisha na
miradi ya mapambano ya Ukimwi zishirikiane na serikali kwa kuyafichua madanguro
hayo kisha kuwapatia elimu wajihusishao na biashara hiyo kwa kuwajengea uwezo
wa kujihusisha na shughuli za ujasiriamali.
Alizitaka Asasi hizo ziwaunganishe machangudoa
katika vikundi vya kijasiriamali huku zikifanyika jitihada za kuwatafutia
mitaji hatua itakayosaidia kuondokana na vitendo vyao vya biashara ya ngono na
kusaidia kupunguza maambukizi ya Ukimwi.
“Madanguro yafichuliwe,na gesti zinazofanya na
kuhamasisha biashara ya ngono zichukuliwe hatua kwakuwa wanafanya jinai,”
Alisema Rufunga. Eti wapo Ofisini
wakisubiri Wateja Awali Mkurugenzi wa miradi wa SHDEPHA+ wilaya ya
Kahama,Venance Mzuka alibainisha kuwepo kwa biashara ya ngono wilayani Kahama
kwa akiana dada wanaojiuza kukodi na kulipia vyumba kwa mwezi mzima katika
baadhi ya Nyumba za kulala wageni.
“Kuna ongezeko kubwa la biashara ya
ngono mjini Kahama kutokana na mji kukua kwa kasi,sababu ikiwa ni uwepo wa
migodi mikubwa na midogo ya madini,huku gesti baadhi zikitumika ambazo siku
zote tangu asubuhi utaambiwa vyumba vimejaa”
,Alisema Mzuka. yupo mawindoni
kusaka mkate wa kila siku Mkoa wa Shinyanga hadi kufikia Juni mwaka huu ulikuwa
na maambukizi asilimia 5.9 huku wilaya ya Kahama ikiwa na maambukizi asilimia
6.1 ambapo Halmashauri ya Mji ikiongoza kwa asilimia 7.8,ikifutiwa na
halmashauri ya Mji wa Kahama kwa asilimia 7.8,Msalala asilimia 5.6 na Ushetu ni
asilimia 5.0. Pamoja na kiwango hicho cha maambukizi imeweka mkakati kufikia
mwakani 2015 uwe chini ya asilimia za kitaifa ambazo ni 5.1.
No comments: