Kamanda wa polisi wa mkoa wa shinyanga (RPC) justus kamugisha akitolea maelenzo ya vurungu zilizotokea mjini kahama ya moja ya mufasi wa chadema kuwauwa na watu wasiofamika .
Mwanamme mmoja aliyefahamika kwa jina
la Simeo Isaka (42),mkazi wa kijiji cha Ngokolo kata ya Bukomela tarafa ya
Mweli wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, ameuawa kwa kukatwa na
jembe kichwani wakati akishangilia matokeo ya ushindi wa mgombea wake kupitia Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa jeshi la
Polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha, alisema tukio hilo limetokea
Desemba 15 majira ya saa saba usiku wakati mwanamme akishangilia matokeo ya uchaguzi
wa serikali za mitaa.
Kamanda Kamugisha alisema, marehemu huyo
alikuwa akishangilia ushindi wa mgombea wa Chama Cha Demokrsia na
Maendeleo (Chadema), ngazi ya mwenyekiti wa kijiji cha Ngokolo kata ya Bukomela
wilayani Kahama.
Kamanda Kamugisha alisema wakati Simeo Isaka
akishangilia ushindi huo ghafla alivamiwa na watu watatu
wasiojulikana kisha kumkata jembe kichwani, na kisha kukimbizwa
katika hospitali ya wilaya ya Kahama ambako alipoteza maisha.
Kamanda Kamugisha
alisema jeshi la polisi linafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo na juhudi za
kuwasaka na kuwakamata watuhumiwa wa tukio hilo zinaendelea ili wachukuliwe
hatua kali za kisheria.
No comments: