Msimamizi mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro,Elias Kilela,akimwangalia mmoja wa majeruhi , Costa Augustino ,mkazi wa kijiji cha Dihombo wilayani Mvomero
Kamanda Mstaafu wa Polisi wa mkoa wa Pwani Ally Ambilikila
na familia yake Januari 16 alipona kufa wakati
alipoonja sekseke la wafugaji jamii ya kimasai akiwa shambani akilima bonde la
Mgongola kuvurugwa baada ya kuvamiwa na wafugaji hao.
Imeelezwa kuwa kamanda huyo ni miongoni mwa wakulima 14
waliojeruhiwa na mmoja kuuawa katika balaa jingine linaloachiwa kuendelea
katika mkoa wa Morogoro.
Bosi huyo wa zamani wa polisi amesema kwa mdomo wake kwamba
pamoja na kukipata cha moto walimpora fedha
taslimu sh: milioni tattu na kuchomewa moto nyumba iliokuwa eneo la
shamba lake.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ,Leonald Paulo,
alithibitisha kutokea kwa mapigano hayo na kumtaja aliyefariki ni Abdallah
shomari(27) mkazi wa Msamvu Manispaa ya Morogoro ambaye alikuwa ndani ya shamba
hilo na kupigwa kwa marungu na wafugaji hao.
No comments: