Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa sokola mary sumuni Kupitia chama cha maendeleo chadema (umarufu Mama mchungaji )akisitiza suala uzoaji wa taka katika Dapo la majengo sokola ofisini kwake na waandishi wa habari .
Mary sumuni mama mchungaji akisisitiza kufanya usafi kwa kuamashisha wananchi wa mtaa wa sokola na mjumbe mwenye kofia chancella sumer akisikiliza maelezo toka kwa mwenyekiti wa mtaa mary sumuni ofisini kwake majengo.
Eneo la Dapo ambalo wakazi wa maeneo hayo ya majengo wakilalamikia Halmashauri ya mji
Baadhi ya kinamama wakitafuta mikaa katika Dapo hilo wakishanga mpiga picha
Mmoja wa wakazi wa eneo la majengo akiwa na ndoo ya uchafu akiwanga nje ya Dapo Baadala ya ndani jala hilo .
Mwenyekiti wa mtaa wa sokola Mary sumuni akionyesha baadhi ya wajumbe wa kamati juu ya uchafu huo huliokidhiri katika eneo hilo .
Eneo la Dapo ilinavyonekana jinsi ilivyotapaka eneo hilo na kusababisha haza kwa wakazi wa eneo hilo .
Mwenyekiti akionyesha jinsi uchafu hulivyotupwa nje ya jala hilo na kuwa kila sehemu .
Haya ndiyo maeneo ya mama lishe ya kuuza vyakula katika eneo hilo jambo ambalo ni hatari kwa afya jamii iliopo maeneo hayo .
Hii ndiyo Bucha ya kuuza nyama eneo la Dapo ambapo limekidhili kwa uchafu na hatari kwa afya .
Hili ndiyo Dapo kama linavyonekana ambapo mjumbe wa kati ya mtaa chancella sumer akiwa juu ya jala hilo na kuonyesha jinsi uchafu huo hulivyotapaka sehemu ya barabarani .
Mwenyekiti wa mtaa mary akionyesha jinsi eneo lilivyo kubwa kwa kila mtu kuwanga uchafu wake kila kona
Mama huyu akiwa na ndoo yake ya kuwanga uchafu.
Mtoto huyu ambaye jina lake alikuwenza kujulikana mara moja akiwa amebeba bakuli lenye uchafu akipeleka kwenye Dapo hilo.
Wananchi wa kata ya majengo wilayani kahama mkoani shinyanga
waomba mkurungezi wa Halmashauri ya mji wa kahama kuondoa Dapo lilipo katika
maeneo ya makazi ya watu.
Hayolisemwa na mwenyekiti wa mtaa wa sokola mary sumuni (Marufu
kwa mama mchungaji alisema Dapo hilo limekuwa kero kubwa katika maeneo hilo kwa
kuahatarisha afya za watu.
Mwenyekiti huyo alizidi kusema kuwa Dapo hilo limefanya
kuzaanga kwa uchafu kila mahara hili si jambo nzuri kwa mfano hapa maeneo kuna
vyakula vya kina mama malishe wanapika vyakula hapa kuna bucha za kuuza nyama
na kuwa eneo hilo kutakuwa salama kwa
maisha ya wanachi wa maeneo hayo .
“Huu uchafu kuwa hapa usipoodolewa na halmashauri mimi
nitaitisha mandamano makubwa ya kuja
kuondoa uchafu na kuweka ulinzi katika eneo hili na tuone kama kuna mtu anakuja
kuweka uchafu hapa,na uchafu huu tutausomba uchafu wote na kupeleka ofisi kwa
mkurungezi”.alisema mwenyekiti wa mtaa wa sokola.
Aidha sumuni alisema kuwa swala la usafi katika maeneo ya
jamii ni la kwetu sote jamii na halmashauri kufanyakazi kwa pamoja kuna mafungu
ya usafi yako wapi mpaka uchafu huu unakuwa kero kwa jamii kila moja anaweka
natupa uchafu sehemu yoyote .
Baadhi ya kinamamalishe wa maeneo hayo salima juma alisema
kuwa Dapo hili limekuwa kero sana hasa katika kipindi hiki cha mvua eneo hili
limekuwa na shida kubwa ya uchafu na harufu mbaya ya kuoza kwa vitu ana
kuhatarisha hata afya zetu na jamii kwa ujumla alisema salima .
Na kwa upande wake mkurungezi wa Halimashauri ya mji felix
kimario alisema kweli Dapo hilo limekuwa kero katika eneo hilo na kwa kuwa
tunasubiri mafungu ilituone jinsi gani ya kuweka suala hilo vizuri.
Aidha kwakuwa hali hiyo imekuwa kero tunaondoa uchafu huo kwa
magari yetu hayo machache ilikupunguza mlundikano huo wa uchafu katika eneo
hilo.
Mwisho
No comments: