Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Tasaf Zuhura Mdungi Akitoa maelenzo kwenye kikao kazi cha waratibu wa mpango ,Maafisa ushauri na usimamizi Na Waandishi wa Habari wa mikoa ya Geita ,Kagera na Geita
Baadhi ya Waandishi wa kiteingo cha habari cha Tasaf kinagho Banduka na Victor Manyai.
Baadhi ya Waandishi wakisikiliza maanda toka kwa kiongozi wa Tasaf Taifa.
Hivi ndiyo hali halisi ya kikao kazi kwa waandishi wa habari kama huyu dada halivyochoka na kazi ya kusikiliza maada .
Waandishi wakiwa makini kusikiliza Maada ya kikao kazi jiji mwanza.
Umakini tunasikiliza
Baadhi ya Waandishi wa habari na viongozi wa Tasaf Taifa na mkoa wa shinyanga wakiwa katika picha pamoja .
Waandishi wa Habari wakisikiliza .
Muandishi wa gazeti la majira Mkoa wa shinyanga Selemani Abeid akisikiliza maada ya kikao kazi cha Tasaf jiji mwanza .
Waandishi wakiwa makini
Wandishi wakifatilia kwa makini
Umakini kwa kusikiliza
VYOMBO vya habari nchini vimetajwa kuwa
na mchango mkubwa katika ufanikishaji wa Mpango wa kuzinusuru kaya maskini
nchini unaotekelezwa kupitia TASAF awamu ya tatu.
Hali hiyo imeelezwa na mkurugenzi mkuu
wa TASAF nchini, Ladislaus Mwamanga katika hotuba yake ya ufunguzi iliyosomwa
kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Ukaguzi, Christopher Sanga katika kikao cha
kazi cha watendaji wa TASAF na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Shinyanga,
Geita na Kagera kinachofanyika jijini Mwanza.
Katika hotuba yake Mwamanga alisema
vyombo vya habari vinategemewa kuwa na mchango mkubwa katika kuihabarisha jamii
ili iweze kuelewe malengo mahususi ya kuanzishwa kwa mpango wa kuzinusuru kaya
maskini nchini na kwamba iwapo jamii itapata habari sahihi itaweza kuutekeleza
vyema mpango huo.
“Kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya
habari, tangu awali TASAF imekuwa ikivishirikisha vyombo hivyo katika utoaji wa
elimu ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa ili walengwa waweze kufahamu
shughuli zetu, lengo la kuwashirikisha ni kuhakikisha mnafikisha ujumbe sahihi
kwa wananchi,”
“Pamoja na kwamba pamekuwepo na
upotoshwaji kuhusu shughuli za TASAF, hususan kuhusiana na utekelezaji wa
Mpango wa Kunusuru kaya maskini, baadhi ya ujumbe unaowasilishwa na baadhi ya
vyombo vya habari siyo sahihi,”
“Hivyo TASAF tumeona haja ya kuandaa
vikao hivi vya kazi kwa nchi nzima ili wote tuweze kujenga uelewa wa pamoja
kuhusu Mpango kwa lengo la kuhakikisha tunafikisha ujumbe sahihi kwa wananchi,”
ilieleza sehemu ya hotuba ya mkurugenzi huyo.
Alisema ushirikishwaji wa jamii na
wadau mbalimbali ni moja ya misingi ya TASAF, hivyo anatarajia kikao hicho cha
kazi kilichowashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari
kitaimarisha ushirikiano kati ya wanahabari na TASAF.
Mkurugenzi huyo alisema TASAF ni chombo
cha serikali na hakifungamani na chama chochote cha kisiasa au kidini na kwamba
lengo kuu la mpango unaondelea hivi sasa nchini ni kuzinusuru kaya maskini kwa
kujenga raslimali watu ya baadaye kwa kuziwezesha kaya hizo katika lishe, afya
na elimu hasa kwa watoto.
“Awali katika awamu zilizotangulia,
TASAF iliweka msisitizo mkubwa katika utekelezaji wa miradi kama ujenzi wa
shule, zahanati na maji kwa lengo la kuhakikisha kaya maskini zinanufaika na
huduma hizo muhimu, lakini tathimini zilionesha kaya hizo hazifaidiki kwa kwa
kiwango kikubwa na huduma hizo,”
“Baadhi ya watoto kutoka katika kaya
maskini walilazimika kufanya vibarua na biashara ndogo ndogo kama kuuza karanga
badala ya kuwa shuleni na baadhi ya kaya hizo hazikuweza kuwapeleka watoto
wadogo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya chanjo na
kufuatilia afya zao,” alieleza Mwamanga.
Alisema mpaka hivi sasa tayari kuna
mafanikio chanya yaliyoanza kuonekana kwa walengwa wamelionufaika na ruzuku
iliyotolewa hususan katika nyanja za elimu, afya, lishe, makazi na hata kuweza
kuwa na shughuli za uzalishaji mali kwenye maeneo yao na tayari kiasi cha
shilingi bilioni 49 zimetolewa kwa walengwa wa mpango huo nchini kote.
"Mafanikio haya yaliyopatikana
yanapaswa kutangazwa ikiwa ni pamoja na changamoto zake ili kuwezesha mfuko
kuboresha zaidi huduma hizi huku walengwa nao wakielimishwa zaidi namna ya
kutumia fursa hii katika kujikomboa kutoka kwenye dimbwi la umaskini,"
alieleza Mwamanga.
No comments: