sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA NA MAHINDI KAHAMA WACHE KILIMO CHA MAZOEA

 Moja ya shamba la mfano katika kijiji cha  Bulima kikundi cha songambele ni shamba la mfano la kikundi .
 Baadhi ya wanakikundi cha songambele wakiangalia zao la pamba ambalo limelimwa kwa hatu za kilimo cha pamba katika kijiji cha bulima.
 Wakinamama wa kikundi cha songambele wakiangali wadudu walibifu wa zao la pamba .

 Afisa kilimo wa makampuni ya ipp  aliainama chini  joseph  mtalamu wa kampuni ya ipp ya umoja wa waunza dawa za kilimo ,kungawa dawa wakiangalia mchi wa zaop la pamba .
 

 kaimu meneja bodi ya Pamba kanda ya Magharibi Buluma Kalidushi alipokuwa akizungumza na wakulima wa vijiji vya Chibiso na Mapamba katika siku ya wakulima shambani alikuja mikono
moja ya shamba la mfano la zao la pamba ambapo afisa kilimo toka makampuni ya ipp joseph akionyesha pamba ilipandwa kwa kufata vipimo .





 shamba la mahindi la mfano
 meneja mradi Focus Laurent akiangalia mahindi yaliyolimwa kwa kufata hatua moja na nyingi ambapo heka moja hutoa jumla maguni 25 mpaka 30 kwa kufata vipimo .

 meneja mradi Focus Laurent akiwaonyesha wakulima wa Bulima kilimo bora kwa kulima kwa wakati na mvua za mwanzo. 
 
Afisa wa bodi ya pamba wilayani kahama mihayo akitoa maelenzo juu ya kilimo bora cha zao la pamba katika kijiji cha Bulima wilayani kahama .  
  Wahamasishaji wa kilimo cha kisasa,kupitia mradi wa Input Promotion Programm(I.P.P) kanda ya magharibi kupitia kwa meneja mradi Focus Laurent akitoa maelenzo juu ya upandaji wa mbengu za mahindi katika kijiji cha chibiso wilayani kahama .

KAHAMA
Wakulima katika halimashauri ya Ushetu wilayani Kahama wameaswa kuacha kilimo cha mazoea  ambacho hakina tija ukilinganisha na hali ya hewa inavyobadilika badala yake watumie njia za kisasa ambazo zitaendana na mahitaji yao ya maendeleo.

Wito huo umetolewa  na kaimu meneja bodi ya Pamba kanda ya Magharibi Buluma Kalidushi alipokuwa akizungumza na wakulima wa vijiji vya Chibiso na Mapamba katika siku ya wakulima shambani ambapo aliwatembelea wakulima hao kwa lengo la  kuhamasisha kilimo cha kisasa kwa wakulima.

Kalidushi amesema wakulima wanapaswa kufuata njia za kisasa kuanzia wakati wa kuandaa mashamba,upandaji,utunzaji wa mazao na kuacha kutumia kilimo kilichozoeleka kwani nyakati za sasa haziendani na awali kulingana na hali ya hewa si kwa mazao ya chakula au biashara.

Kwa upande wao wahamasishaji wa kilimo cha kisasa,kupitia mradi wa Input Promotion Programm(I.P.P) kanda ya magharibi kupitia kwa meneja mradi Focus Laurent amesema watashiriki na kuwaelimisha wakulima kufuata njia bora za kilimo cha kisasa.

Nao badhi ya wakulima wa vijiji vya Chibiso na Mapamba Charles Ng’imba na Pellagia Simon ambao mradi huo wa I.P.P unaotekelezwa kwao wamewashukuru mafunzo wanayopatiwa kwani kilimo cha njia bora za kisasa zinawaletea mavuno mengi tofauti na awali.

Input Promotion Programme(IPP) ni  mradi wenye lengo la kutoa elimu ya njia bora za kisasa za kilimo upo chini ya makampuni yaYARA,SEEDCO,QUITON,BAYER,TGT,na unatoa huduma hiyo katika mikoa ya Simiyu,Maswa,Kahama,Geita,Tabora  Mara.na kagera

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply