sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » LUKUVI ZIPELEKENI OFA ZENU MPEWE HATI KAMILI


 Na mohab Dominick
May 2,2015
Kahama 
LUKUVI ataka wananchi kuzisalimisha ofa zao.

WAZIRI wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi amewata wananchi wanaoendelea kutumia ofa za viwanja zilizo futwa wajisalimishe katika ofisi za ardhi kabla hawajachukuliwa hatua ili zihakikiwe na ikibainika ni za kweli wapatiwe hatimiliki.

Hayo aliyasema mwishoni mwa wiki  wakati akizungumza na wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga   alipokuwa katika ziara yake ya kikazi huku lengo ni kutatua kero ya ardhi ambayo imezidi kushamili katika mji wa Kahama.

Wazili huyo aliwataka wakazi wa mji huo kama bado wanaendelea kutumia Ofa za viwanja  zilizofutwa na serikali  wajisalimishe katika ofisi za ardhi  kabla  hawajachukukuliwa hatua ili zihakikiwe na ikibainika ni za kweli wapewe hati miliki.

"Wanaoendelea kutumia ofa wakati serikali imeshazifuta tafadhali nawataka wajisalimishe wenyewe kwenye ofisi za ardhi mji wa Kahama ili zihakikiwe kama ni za kweli,na zitakapo bainika  ni za kweli siyo mlipewa mabomu mpatiwa hati miliki la sivyo sheria itachukua mkondo wake kwani ofa zilisha futwa muda murefu sana,"alisema Lukuvi.

Pia Lukuvi aliwaeleza wananchi kuwa katika ziara yake aliyotembelea maeneo mengi yenye migogoro katika mji wa Kahama amebaini kuwa migogoro hiyo inasababishwa na watendaji wa kata na vijiji pamoja na maafisa ardhi wenyewe kutowahusisha wananchi ili kupata maoni yao juu kwakuwa ndiyo wahusika wa maeneo yanayopimwa.

"Katika ziara hii nimejionea mwenyewe na siambiwi na mtu hali ya migogoro katika maeneo mengi ya mji huu inasababishwa na watendaji wa kata na vijiji pamoja na maafisa wa ardhi wanapofika kwenye vitongoji kwenda kupima ardhi hawawashirikishi wananchi wa maeneo husika ambao wanajua kila kiltu badala yake wanatumia watendaji ambao wengi wao huwa ni wababe,"alisema na kuongeza.

"Ni marufuku maafisa ardhi kuwamilikisha ardhi wananchi kwa kutumia ofa, pia watumishi wa  ardhi nawaagiza kuanzia sasa mnapofika kwa wananchi kupima ardhi lazima mpite kwa wenye viti wa vitongoji ili wananchi wa maeneo husika waweze washilikishwa itasaidia kuepuka migogoro,"alisema.

Pia Lukuvi ameiagiza serikali wilayani humo kushirikiana na Halmashauri zake katika kutenda haki kwa wananchi na kuwaomba wananchi kuwaepuka matapeli wanaojifanya kuwa ni watumishi wa idara ya ardhi badala yake wafike katika ofisi za ardhi ikiwa ni pamoja na kutokubali kupewa ofa za viwaja kutokana na serikali ilisha futa kwani hali iliyopo sasa ni kupatiwa hati miliki.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya alisema kuna wimbi kubwa la matapeli wa ardhi ambao awali walifanya kazi katika idara hiyo na asilimia kubwa wananchi walio wengi bado wanawaamini hali inayosababisha kukithili kwa  migogoro ya arhi katika Wilaya ya Kahama.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply