Ikiwa ni
siku kadhaa tangu headline za Umoja wa vyama vya katiba nchini (UKAWA)
kutangaza kuwa havitashiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar unaotarajiwa
kufanyika March 20 2016, Leo March 17 2016 headline nyingine ni kutoka
kwa Vyama visivyo na uwakilishi bungeni ikiwa ni pamoja na DP, CCK, SAU,
AFP, TLP, ADA TADEA, UPDP, D. MAKINI, NRA, UMD, CHAUSTA na ADC vimetoa
yao ya kauli yao kuhusu ucchaguzi huo na kusema vitashiriki kwa kufuata
sheria ya uchaguzi ya mwaka 1984.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es salaam, Katibu mkuu wa chama cha DP Abdul Mluya amesema ‘Vyama
vyetu vianatambua kuwa, chombo chenye mamlaka ya kutangaza tarehe ya
uchaguzi kwa mujibu wa sheria ni ZEC na ndio chenye mamlaka ya
kumtangaza mshindi aliyeshinda kwa kura nyingi‘
‘Vyama
vyetu vimeona kuwa kwa kua vyama hivi vilishiriki uchaguzi kwa nafasi
ya Rais oct 25, 2015 vilikuwa 14 vikiwa na imani na tume ya uchaguzi‘ ;-Abdul Mluya
‘kwa
imani hiyo ndio maana vyama hivi vilishiriki uchaguzi huo wa
awali,hivyo hatunabudi kushiriki uchaguzi huo ili demokrasia ishike
mkondo wake na hatimaye mshindi apatikane kwa njia ya kidemokrasia‘ ;-Abdul Mluya
Kwa hisani milladayo
No comments: