KAMATI ya ulinzi na Usalama wilaya ya Nyang’hwale mkoa wa Geita imetishia kuyafunga machimbo mapya
yaliyoibuliwa na wachimbaji wadogo katika kijiji cha Nundu baada ya wachimbaji kumkataa
mwekezaji wa kampuni ya Busolwa mining Baraka Ezekiel badala yake wanataka
wafanye na kampuni ya Bismark hoteli iliyotamburishwa kwao.
Wachimbaji hao wamedai kuwa wapo tayari kufanya kazi na mwekezaji
halali aliyetamburishwa kwao na serikali ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Bismark
hoteli anayedaiwa kumiliki leseni ya utafiti katika eneo hilo na kuongeza kuwa hawapo tayari kufanya kazi
na mwekezaji mwingine waliemtaja kwa jina la Baraka Ezekieli anayemiliki
kampuni ya Busolwa mining anayeonekana kusimamia suala hilo.
Kamati hali isiyokuwa ya kawaida nipashe kimeshuhudia kamati
ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo iliyoongozwa na afisa tawala wa wilaya hiyo
Manyonyi Manyonyi huku jeshi la polisi likiwa limebeba siraha nzito
zilizosheheni risasi za moto na mabomu ili kuweka hali ya ulinzi na usalama kwa
wananchi wa eneo hilo.
“Sisi kama wachimbaji
wadogo hatuna shida na Bismark tupo tayari kufanya kazi naye lakini hali
imekuwa tofauti na jinsi tulivyotarajia, kwani tunayemuona kufika mara kwa mara
katika eneo letu ni Baraka anayemiliki kampuni ya Busolwa mining na amekuwa
karibu sana na serikali ya wilaya hatupo
tayari kufanya naye kazi hizi kama
atakuja Bismarck mwenyewe hakuna tatizo na ni lazima tukutane naye mwenyewe
hata siku zanyuma tuliambia hivi hivi huko machimbo ya Lyulu alitufukuza na
sasa tumerudi hapa napo anapataka ni maelfu ya watu tupo hapa hatumtaki kabisa
tumegundua wenyewe,” alisema mchimbaji aliyejitamburisha kwa jina la Elias Maliganya.
Pia wachimbaji hao wamesema kuwa kila wanapogundua madini ya
dhahabu mwekezaji huyo hudai ni maeneo yake na kusababisha wachimbaji wadogo
kufukuzwa na serikali katika maeneo hayo
kwa madai wamevamia leseni ya mtu jambo ambalo ni uonevu mkubwa na kunyanyaswa
wachimbaji hao.
“Tunamuomba Rais Magufuri atusaidie sisi wachimbaji wadogo tuna
nyanyasika kwa wawekezaji wakubwa hapa wilayani kwetu wandishi hawa maelfu ya watu tulikuwa katika
machimbo ya Lyulu ambako tulifukuzwa na huyu mwekezaji anayekingiwa kifua na
serikali ya wilaya, tukakubali tukamwachia eneo baada ya kuvumbua tena dhahabu
katika kijiji hiki cha Nundu kaletwa tena na serikali eti kwa kivuli cha
Bismark hotel ndiyo maana tumemuomba Bismark tukutane naye lakini kama Baraka
hatupo tayari,” alisema mchimbaji mwingine Mrisho Shashu.
Wachimbaji hao waliendelea kusema kuwa mwekezaji huyo waliyemtaja
kwa jina la Baraka Ezekieli anajinufaisha kupitia wachimbaji wadogo kwa kudhulumu
maeneo wanayovumbua wenyewe na kwamba pindi wanapogundua maeneo yenye madini ya
dhahabu yeye hutumia jeshi la polisi na mkuu wa wilaya kuwaondoa katika maeneo hayo
jambo ambalo wanamuomba rais kuingilia kati na kumdhibiti mwekezaji huyo.
Katika hatua nyingine mmoja wa wamiliki wa mashamba Charles
Luchanganya alisema katika kikao chao kilichojumuisha wamiliki wa mashamba,
Mwekezaji pamoja na mkuu wa wilaya hiyo kilichofanyika ofisini kwake walidai
kulazimishwa na mkuu huyo wa wilaya kusaini makubaliano ya wao kushirikiana na
mwekezaji jambo ambalo walisema hawajatendewa haki.
Akijibu malalamiko hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari
waliofika ofisini kwake mkuu wa wilaya hiyo Hamim Gwiyama alisema kuwa amepokea
barua kutoka wizara ya Nishati na Madini inayoeleza kwamba Bismark
ilihamisha umiliki wake wa hizo leseni kwa
kutumia sheria ya Madini ibara no.9
hivyo ni eneo lake kwa mujibu wa Barua ya tarehe 17/03/2017.
“ Sasa kama mtu amepata haki yake kwa mujibu wa sheria utamtoa
kisa jina la Baraka ama? ipo barua hapa mezani kwangu imetoka wizara ya Nishati
na Madini inakwenda ofisi ya kijiji cha Lyulu Kata ya Nundu ikijibu malalamiko
ya wachimbaji hao na mimi nasimamia vizuri agizo hilo,” alisema Gwiyama.
Akizungumzia kuhusu suala la kumpa ulinzi wa jeshi la polisi
mwekezaji huyo Gwiyama alisema kuwa kila mtanzania anayo haki ya kupewa ulinzi
isipokuwa asivunje sheria za nchi na kazi ya serikali ni kuhakikisha suala la
amani linaimarika maradufu.
Kwa upande wake mwekezaji wa kampuni ya Busolwa mining Baraka
Ezekiel akizungumza na wandishi wa habari alisema kuwa yeye anafanya kazi za
uchimaji wa madini ya dhahabu kwa kushirikiana na kampuni ya Bismark hoteli
hivyo kwa kuwa wachimbaji wamekataa kushirikiana naye ataiomba serikali ione
umuhimu wa kuwaondoa hao watu waondoke kwa nguvu katika eneo hilo.
“Kinachofanyika pale kuna ugomvi wa kibiashara kuna watu wanaojiita makota, makota hao hawa
utaratibu wao huwa hawataki kufuata sheria, wao wanataka maslahi kama jana
wamenunua mfuko mmoja kwa shilingi
milioni 1.2 wenye gramu 300, sawa na milioni 28 sasa hawalipi kodi mimi
nitalipa kodi na nilikubali tushirikiane nao na tukawapa asilimia 60 kwakuwa
wamekataa wataliacha eneo hilo,” alisema Ezekieli mwekezaji.
Naye afisa mtendaji wa kijiji cha Nundu, Juma Madinda akizungumza
na wandishi wa habari waliotaka kujua uhalali wa mwekezaji huyo alisema kijiji
hakimtambui kama mwekezaji wa maeneo hayo na kijiji hakina nyaraka zinazoonesha
kumbu kumbu isipokuwa anafahamu hivi karibuni aliketi katika kikao cha
halmashauri ya kijiji na kukosekana maelewano.
“Kama mtendaji wa kijiji husika sina nyaraka zinazoonyesha leseni
japokuwa inadaiwa kuna leseni ya utafiti kwenye kijiji changu pia natambua
wachimbaji wamevumbua madini kwenye mashamba ya familia mbili tofauti familia
moja ni familia yam zee Luchanganya Nguguta na familia ya Mzee Emmanuel kulwa
na hawa wapo zaidi ya miaka 60 sasa siwezi kumtambua wakati sijaona hata
nyaraka moja na baada ya kuibuka kwa machimbo haya hakuna hata familia moja
iliyoleta malalamiko kuvamiwa na wananchi wanaochimba,” alisema Madinda.
WACHIMBAJI WADOGO WAKIENDELEA NA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI |
MASHAMBA YA WANANCHI KU WALIOVAMIWA NA WACHIMBAJI WADOGO |
KIKOSI CHA JESHI LA POLISI WILAYANI NYANG'HWALE KILICHOAMBATANA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA KIKITULIZA GHASIA KWA WACHIMBAJI WADOGO |
MMOJA WA WACHIMBAJI AKIDHIBITIWA NA JESHI LA POLISI |
MWANAMKE AKICHIMBA MADINI SEHEMU WALIYO VUMBUA WENYEWE |
No comments: