Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, anatarajia kufanya ziara rasmi ya siku tatu kuanzia tarehe
05,Juni, 2017 Mkoani Mara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa kitengo cha habari
na Mawasiliano mkoani huo inasema, Mhe Samia atatembelea Wilaya ya
Tarime, katika Kituo cha Afya cha Nyamwaga kinachojengwa na wananchi kwa
msaada wa Mgodi wa Acacia North Mara.
Pia, Mhe. Makamu wa Rais atapata fursa ya kutembelea Bonde la Mto
Mara kunakokusudiwa kuanza kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha
sukari. Mchana siku hiyo hiyo atafanya mkutano wa hadhara katika Kijiji
cha Bisarwi; katika eneo hilo kunakusudiwa kujengwa kiwanda cha sukari.
Aidha tarehe 6/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais ataenda Wilaya ya Serengeti
ambapo ataweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Wilaya, mchana
atafanya Mkutano wa Hadhara katika Uwanja wa Mbuzi, Mugumu mjini.
Tarehe 7/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais atakuwa Musoma ambapo ataweka
jiwe la msingi kwenye barabara ya km.9.9 inayojengwa kwa kiwango cha
lami katika Manispaa ya Musoma. Pia atatembelea kiwanda cha Samaki cha
Musoma Fish Processors (T) Ltd na kufanya Mkutano wa Hadhara katika
uwanja wa Mukendo Musoma Mjini.
Hii ni mara ya kwanza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa na ziara rasmi Mkoani Mara.
habari
Habari Za Mastaa
Michezo
simulizi za kusisimua
MOHABMATUKIO.BLOGSPOT.COM's Admin
We are.., This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Post
-
Eneo la mbele la shule la ROCKEN HILL ACADEMY karibu sana kwa elimu bora kwa mtoto wako Ramani ya afrika katika eneo la shule ...
No comments: