Moja ya Bomu la kutupwa kwa mkono aliokamatwa nayo Aisha juma mkazi wa kata ya nyahanga wilayani kahama |
Pingu ambazo alikamatwa nazo Aisha juma |
Risasi alizokamatwa nazo Aisha juma mkazi wa kata ya nyahanga wilayani kahama pamoja na mabomu ya kutupa kwa mkono KAHAMA |
Mahakama wilaya ya kahama mkoani shinyanga imehukumu kifungo cha
miaka 10 Aisha Juma kwa
kosa la kuutwa na hatia ya kukamatwa na siraha mabomu ya kutupa na mkono pamoja
visu na pingu katika kata ya nyahanga.
Akiongea mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Vodia Kiharuzi mwendesha mashitaka
Athumani kisango aliambia mahakama hiyo kuwa Aisha juma alikamatwa maeneo ya
nyahanga majira ya joni akiwa na silaha hizo.
Aidha mwendesha mashitaka aliambia mahakama aisha alikamatwa
tarehe 11 mwezi wa kumi nyumbani kwake akiwa na silaha hizo,kwa mujibu wa
sheria cha 21 cha mwaka 2015 ni kosa kukutwa na risasi.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga,Evodia Kyaruzi
alisema kuwa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri
ameridhika kuwa, mshitakiwa walikutwa na mabomu hayo ya kinyume cha sheria na kumtia
hatiani kwenda jela mika kumi .
Hakimu huyo alisema kuwa,mahakama hiyo baada ya kupitia ushahidi
uliotolewa na pande zote imeridhika nao, hivyo washitakiwa wanatiwa hatiani kwa
kifungo cha adhabu ya sheria cha 21 cha mwaka 2015.
Awali
katika ushahidi wake Mwendesha mashitaka wa polisi upande wa Jamhuri, Athumani kisango na upande wa mashahidi
uliotolewa mahakamani hapo waliiambia mahakama hiyo
kuwa,mshitakiwa walikutwa na mabomu hayo katika eneo la nyahanga .
Kwa upande wake mshitakiwa katika utetezi
wake,alikana kukutwa na mabomu hayo kuomba
mahakama kupunguzia adhabu hiyo.
Awali katika kesi hiyo Mwendesha mashitaka wa polisi upande wa
Jamhuri Athumani
kisango ,aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe
kufundisho kwa jamii na watu wenye kujihusisha na biashara za kuuza siraha.
Mwisho
No comments: