sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WAZEE KAHAMA WAMPONGEZA JPM DHIDI YA MAKINIKIA

 Katibu wa umoja wa wazee kahama Uwaka Paul Ntelya akisoma tamko la wazee kwa kupongeza juhudi za mh Rais John Magufuli 

Mwenyekiti wa umoja  wa Uwaka  Batholomeo Kayoka

 Viongozi wa vyama vya upinzani wakiwasikiliza umoja wa wazee wa kahama kwenye kikao cha kumpongeza Rais Magufuli kwa uwamuzi wa kuzuia mchanga wa makanikia 

 Baadhi ya wazee kinamama wakiwa katika kikao 

Wazee 

 Mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya kahama Joel Marunga akiwa na mwenyekiti wa umoja wa wazee Uwaka kayoka wakati wa kikao cha wazee 

 Tunasikiliza 

 Wazee makini kusikiliza Hotuba na pongeza 

Mkuu wa  kituo cha polisi  kahama akisalimiana na wazee walipofika kwenye kikao chao 
KAHAMA 

UMOJA wa wazee katika halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga (UWAKA) wamempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa harakati anazozifanya na hatua alizochukua baada ya kupokea ripoti ya pili ya uchunguzi wa Makinikia ya mchanga wa Dhahabu.

Akitoa pongezi hizo katika mkutano wao  wa hadhara katibu wa Uwaka , Paul Ntelya alisemasema kuwa pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya wazee wameitaka migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi kulipa deni la shilingi Bilion 17 za Ushuru wa huduma fedha ambazo  hazijalipwa tangu kipindi cha mwaka 1998 hadi 2012.

Katibu wa umoja huo Paul Ntelya aliwaeleza wazee hao kuwa tukio la Juni 12,mwaka huu la Rais Magufuli kufanaya jambo ambalo halikutarajiwa liligusa hisia za kila mtanzania hususani mpenda maendeleo ya kweli hivyo maamuzi yake ya kuzuia kusombwa au kusafirishwa makinikia ya mchanga wa Dhahabu na kuyapeleka nje ya nchi.

Ntelya alisema kuwa mchanga huo ulikuwa unasafirishwa na kampuni ya Acacia inayomiliki migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi tangu kipindi cha mwaka 1998 hadi 2017  kwa mgodi wa Bulyanhulu huku Buzwagi nayo ikisafirisha mchanga huo kuanzia kipindi cha mwaka 2001 hadi mwaka huu 2017 jambo ambalo alidai kuwa liliwasisimua na na kutoa mwanga mpya wa matumaini   ya maendeleo chanya na wananchi waanze kujitambua.

“Wazee wenzangu tumeona ni vyema tukutane kwa dharula hii ili tumpongeze sana Rais wetu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli na kumpa moyo wa aendelee kutufumbua macho ili tupate maendeleo ya kweli, Wazee wenzangu tukirejea hata hotuba ya mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige aliyoitoa Bungeni tarehe 25,05,2013 alipokuwa anachangia hoja  katika bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka wa fedha 2013/2014,” alisema Ntelya.

Alisema mgodi wa Bulyanhulu ulioanza uzalishaji wa Madini ya Dhahabu tangu 1998 na mgodi wa Buzwagi ulioanza uzalishaji mwaka 2001 kwa pamoja hadi 2012 zilizalisha na kuuza Madini yenye thamani ya Dola za kimarekani Bilioni 3.781 ambazo ni sawa na fedha za kitanzania shilingi Trilioni 5.577, hivyo kwa uzalishaji na mauzo hayo Migodi hiyo ilipaswa kulipa mrahaba kwa halmashauri ya Wilaya ya Kahama kabla ya kugawanywa na kupatikana halmashauri tatu.

Aliongeza kuwa Dola za kimarekani milioni 11.15 ambayo ni sawa na shilingi Bilioni 17 za kitanzania hadi leo kampuni hizo hawajafanya malipo yoyote licha ya kwamba wanalitambua hilo na kudai Mbunge Maige aliwahi kuwapelekea nakala ya hotuba yake mwaka 2014 akiwaomba msaada wazee hao waweze kupiga kelele serikalini ili fedha hizo zilipwe kwenye Halmashauri kwa maendeleo ya wananchi.

Nao baadhi ya wazee wamempongeza Rais Magufuli huku wakidai kuwa wakienda Hospitalini kwaajili ya kupatiwa matibabu wanaambulia parasetamu kwa ukosefu wa dawa hivyo Rais Magufuli anapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kuwataka wananchi waungane kwa pamoja ili wamuombee azidi kupambana kwani ni shujaa wa Tanzania.

“ Ni kweli wazee wenzangu kwakweli hili la kumpongeza mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa hii anayotufanyia watanzania sijui kama kuna Rai mwingine atakuja kufanana na huyu naweza kusema huyu kaletwa na Mungu, ningewashangaa sana kuona sisi wazee tunaoishi jilani na migodi hii inayoongoza kwa kusafirisha Michanga ya Dhahabu kwenda nje tunachelewa kumpongeza rais kwani anachokifanya ni kututetea hasa sisi chimbuko la Madini,” alisema mzee Khamis Majid.

Kwaupande wake Mwnyekiti wa umoja huo Batholomeo Kayoka aliwataka wazee hao kuungana kwa pamoja na kuwa namwitikio hasa pale wanapotakiwa kutoa ushauri wao kama wazee.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply