Mtuhumiwa wa wizi wa kuvuja maduka na nyumba za watu Antony Boniphace (21) |
Baadhi ya mmagunia ya bagi kati ya kumi yalikamatwa nyumbani kwa Makongolo Mafundo (32) |
Mkuu wa upelelezi wilaya ya kahama Georger Bagemu akionyesha baadhi ya maguni ya bagi kati ya kumi |
Magunia ya Bagi ambayo yamekatwa na jeshi la polisi kahama |
Magunia ya bagi yakiwa katika kituo cha polisi kahama |
KAHAMA
JESHI la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga linamshikilia Makongolo Mafundo (32) mkazi wa kijiji cha Sigili tarafa ya Itobo Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora kwa kosa la kukutwa na magunia 10 ya bagi yenye ujazo wa kilo 350.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Murilo Jumanne Murilo amedhibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Juni 12 mwaka huu akiwa nyumbani kwake baada ya kukutwa na magunia kumi ya bangi.
Kamanda Murilo alisema kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo nyumbani kwake huko katika kijiji cha Sigili kilichopo mpakani mwa Isaka Wilaya ya Kahama na Nzega Mkoani Tabora baada ya kukutwa na kidhibiti cha magunia hayo ya bangi.
Aidha Kamanda huyo alisema kuwa baada ya jeshi la Polisi mkoani humo kumbana mtuhumiwa huyo alitaja sehemu anakotoa bangi hizo kuwa ni Mambali Nzega mkoani Tabora na kutaja asilimia kubwa ya wateja wake wanatokea jijini Mwanza na bangi hizo zilikuwa tayari kwa kusafirishwa kwenda Mwanza.
Alisema katika Tukio hilo pia nyumbani kwa mwanamke mmoja mkazi wa maeneo hayo aliyefahamika kwa jina la Pili Kizota Polisi wamekuta Bangi magunia makubwa 4, na debe 4 zilizotelekezwa ndani huku mtuhumiwa akitokomea kusiko julikana.
Kamanda Murilo ameapa kuendeleza msako mkali dhidi ya watu wanaoendelea na biashara ya madawa ya kulevya katika Mkoa wake wa Shinyanga.
Wakati huo huo Murilo alisema kuwa watu watatu akiwamo na aliyejidai ni usalama wa Taifa wanashikiliwa na jeshi la Polisi wilayani Kahama kwa uchunguzi wa makosa yao kisha watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
No comments: